Mratibu wa hafla hiyo,Dina Marios kutoka Dada Dina Cares (pichani Mbele),akiwa sambamba na baadhi ya Wadau waliojitokeza kuifanikisha hafla hiyo ya chakula cha mchana na watoto Yatima kutoka vituo vitatu,kushoto ni Dada Janet Sosthenes Mwenda wa Ongea na Janet na wadau wengineo.

Mratibu wa hafla hiyo,Dina Marios
kutoka Dada Dina Cares akiongea na Watoto kutoka vituo Yatima,kabla ya kukata
keki na kuwalisha.

Mratibu wa hafla hiyo,Dina Marios
kutoka Dada Dina Cares akimlisha keki mmoja wa watoto waishio katika mazingira
Magumu kutoka kituo cha Watoto yatima cha Vetenari
Temeke.


Baadhi ya watoto kutoka vituo vya watoto
Yatima,kituo cha Sifa Bunju,Zaidia Sinza pamoja na Vetenari Temeke,wamekutana
leo mchana kwenye Fukwe ya Azura Beach Kawe kwa ajili ya kupata chakula cha
pamoja na watoto wengine,huku michezo mbalimbali kama vile face painting,jumping
castle,kuogelea,kuvuta kamba,mpira wa miguu,kucheza mziki n.k.Michezo hiyo
iliyoandaliwa na Kids Event na mingineyo ilitawala na kuwaburudisha sana
watoto.
Aidha mratibu wa hafla hiyo,Dina Marios
kutoka Dada Dina Cares,amesema kuwa mkusanyiko huo unafanyika kufuatia zoezi
zima la kukamilisha ule mpango ulioanza wa kuchangia vituo vya watoto
yatima.
Pamoja na hafla hiyo pia Keki iliyoandaliwa
na flying chefs ilikatwa huku wasanii mbalimbali wakishiriki kwa pamoja,akiwemo
Shilole,Snura,Quenn Darlin,Mwasiti na wengineo.Janet Sosthenes Mwenda wa Ongea
na Janet na Wasanii wengine walijitolea kuwahudumia na kuwaangalia
watoto.
Dina Marios anawashukuru watu wote
walioshiriki kuchangia vituo hivyo.Wadau wa blog yake
www.dinamarios.blogspot.com wasikilizaji wa leo tena ya clouds fm na wote
walioguswa. Mpango huo utaendelea siku nyingine tena maana ni
endelevu.
Post a Comment