TAMKO RASMI LA UCHAGUZI MDOGO
WA VIONGOZI TAWI LA CCM
WASHINGTON DC, MARYLANG&
VIRGINIA (DMV)
Chama Cha Mapinduzi Tawi la DMV kinapenda
kuwafahamisha wanachama wake wote kuwa kutakuwa na uchaguzi mdogo wa wajumbe
(10) wa Halmashauri kuu ya Tawi.
Kwa mwanachama yeyote yule anayetaka kugombea
nafasi hizo zilizotajwa hapo juu, tafadhali usisite kuwasiliana na katibu wa
tawi, Ndugu, Yacob Kinyemi ( 202) 629- 7841 kwa ajili ya kujipatia fomu za
kugombea uongozi.
Mwiso wa kurudisha fomu ni tarehe August
18,2013. Tarehe ya kufanyika uchaguzi, muda na mahali pakufanyikia uchaguzi
mtatangaziwa katika siku zijazo.
UTARATIBU WA KUGOMBEA
Mwanachama yeyote wa CCM anaweza kugombea nafasi
hizo. Uwe na umri usiopungua miaka 18 ya kuzaliwa. Ili kugombea nafasi yoyote ya
mjumbe wa Halmashauri kuu ya tawi ni lazima uwe na kadi ya uanachama wa ccm. Kwa
wale ambao kadi zao zimepotea, utaratibu wa kupata kadi nyingine upo, tafadhali
wasiliana na katibu wa tawi, Ndugu, Yacob Kinyemi.
UTARATIBU WA KURUDISHA FOMU
Tafadhali tuma fomu yako na ikiambatanishwa na
picha mbili (passport size).
Rudisha fomu yako katika njia ya mawasiliano
haya:
1327 Emerson street Apt# 303 NW
Washington, DC 20011
TARATIBU ZA KUPIGA KURA
Kila mwanachama wa ccm ana haki ya kupiga
kura.
Kupiga kura ni kwa kutumia kadi ya CCM.
Tafadhali wanachama wa CCM, mnaombwa mjitokeze
kugombea nafasi hizo.
Kidumu chama cha mapinduzi
VIFAA VYA WANACHAMA
Ndugu wanachama na wakereketwa wa ccm, mashati,
kofia,skafu, kadi za umoja wa vijana na wazazi, pia zinapatikana, tafadhali
usisite kuwasiliana na uongozi wa tawi, ili uweze kupatiwa vifaa hivyo kwa
haraka iwezekanavyo.
FARAJA ISINGO-KATIBU WA FEDHA NA
UCHUMI:3015927581
SALMA MOSHI-KATIBU MWENEZI NA
ITIKADI:3014011547
GRACE MGAZA-M/KITI UMOJA WA
WAZAZI:2022711860
GRACE MLINGI- KATIBU UMOJA WA
VIJANA:2404291789
Katibu na mkurugenzi mkuu wa uchaguzi,
Tawi la ccm- DMV
Marekani YACOB KINYEMI
Post a Comment