Mbunge
wa Jimbo la Segerea, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk.
Makongoro Mahanga akiwaonesha wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya
ya Ilala (Jimbo la Segerea), kituo kipya cha Polisi cha Tabata, Dar es
Salaam, walipokuwa kwenye ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa
miundombinu jimboni humo.
Dk.
Makongoro Mahanga na Diwani wa Kata ya Tabata, Mtumwa Mohamed pamoja na
wajumbe wakikagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa manne akatika Shule
ya Msingi Tabata
Dk.
Mahanga akitoa maagizo kwa watendaji wa Kata ya Kimanga, kuhakikisha
wanabomoa haraka msingi wa bendera ya CHADEMA, uliojengwa kwenye eneo la
Stendi ya Dcaladala ya Kimanga inayotarajiwa kufanyiwa matengenezo wiki
hii.
Dk. Mahanga akizungumza wakati wa kukagua ujenzi wa daraja la maji ya chumvi.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Ilala, wakikagua maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kinyerezi- Segerea.
Mhandisi wa Manispaa ya Ilala, Muhinda Kassim akitoa ufafanuzi kuhusu maendeleo ya ujenzi wa miradi
Mkazi
wa Kinyerezi akitoa ushauri kwa wahandisi wa Tanroads Dcar es Salaam
kuhakikisha wanatunza vizuri barabara ikiwemo kuwela alama.
Mmoja wa wahandisi wa Tanroads akielezea kuhusu maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kinyerezi-Segerea
Wajumbe wakiwa site ya daraja hilo
Dk. Mahanga akizungumza na wahandisi wa Tanroad Mkoa wa Dar es Salaam.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ilala, wakikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Tabata-Liwiti.
Mhandisi Mwandamizi wa Tanroads DSM, Eliakim Tenga akielezea kuhusu maendeleo ya ya ujenzi wa barabara ya Tabata-Liwiti.
Msafara
wa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ilala, ukiwa kwenye
magari ukikagua maendeleo ya ujenzi wa Barabara ya Liwiti-Baracuda.PICHA
ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG.
Post a Comment