Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

HII HAPA PROGRAMU YA UENDELEZAJI MIJI TANZANIA

               


Picture 237 fc296
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Rebbeca Kwandu(KUSHOTO) akieleza kwa waandishi wa habari kuhusu mapango wa uendelezaji Miji Tanzania katika mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam KATIKATI ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa na KULIA ni Mratibu wa Mradi wa Uendelezaji wa Miji Mkakati Tanzania Kutoka ofisi hiyo Mhandisi Nanai Nyariri.
hdg
 
 
 
PROGRAMU YA UENDELEZAJI MIJI TANZANIA CHINI YA OWM-TAMISEMI
Tanzania imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali za maendeleo ya miji zikiwemo (i) ongezeko la watu kwa kasi mijini; (ii) miundombinu isiyokidhi mahitaji ya miji; (iii) uwezo mdogo wa kifedha kwa ajili ya kutoa huduma za jamii na (iv) usimamizi dhaifu wa maendeleo ya miji katika Halmashauri zake. Inakisiwa kuwa hadi mwaka 2030 asilimia 38 ya watu na takribani watu milioni 25 watakuwa wanaishi katika miji.

Katika Hotuba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete wakati akifungua rasmi Bunge Jipya la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dodoma tarehe 30 Desemba 2005 alieleza juu ya dhamira ya Serikali katika kuboresha miji yetu. Nanukuu
"Kuendeleza miji ni jambo tutakalolipa uzito unaostahili ili tuwe na miji mizuri, safi na salama. Serikali ya awamu ya Nne itazitaka Halmashauri zote zishughulikie jambo hili haraka iwezekanavyo".
Hivyo, kwa kutambua changamoto za miji zinazotukabili, OWM-TAMISEMI ikishirikiana na wabia mbalimbali wa maendeleo, ikiwemo Benki ya Dunia, imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kukabiliana na changamoto hizo. Hatua hizo ni pamoja na kutekeleza miradi mbalimbali. Miongoni mwa miradi ambayo hivi sasa inatekelezwa na OWM- TAMISEMI ni mradi wa Uendelezaji wa Miji Mkakati Tanzania ambao kwa kifupi unajulikana kama Tanzania Strategic Cities Project (TSCP) na Programu ya kuimarisha Halmashauri za Miji – Urban Local Government Strengthening Programme (ULGSP). Aidha maandalizi ya Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP) ambao ni mahsusi kwa Halmashauri tatu (3) za Dar es Salaam nao yanaendelea
Mradi wa Uendelezaji wa Miji Mkakati Tanzania-TSCP, ambao ni mkopo wa Banki ya Duniana DANIDA, umegharimu Dola za kimarekani, Milioni 175.5, ambapo Dola Milioni 163.2 ni kutoka Benki ya Dunia na Dola Milioni 12.2 ni kutoka DANIDA. Mradi unatekelezwa katika miji 7 ya Tanzania Bara ambayo ni Arusha, Dodoma, Kigoma, Mbeya, Mtwara, Tanga na Mwanza. Kwa Dodoma mradi huu unatekelezwa na Manispaa ya Dodoma na Mamlaka ya Ustawishaji wa Makao Makuu Dodoma (CDA).
Mradi huu unalenga kuboresha Huduma za msingi katika miji hii. Lengo hili litafikiwa kwa (i) Kuboresha Miundombinu kama barabara, maeneo ya kutupia taka ngumu, vituo vya mabasi na malori na kununua vifaa vinavyosaidia kudhibiti taka ngumu (ii) Kuimarisha uwezo wa kitaasisi katika uendelezaji na usimamizi wa Miji, Usimamizi na Utunzaji wa mali za Halmashauri, usimamizi na ukusanyaji Mapato kutokana na huduma muhimu za kijamii, uboreshaji wa ukusanyaji wa mapato pamoja na kuboresha mipango miji. Mradi huu ulianza kutekelezwa mwaka 2010 na unategemea kukamilika mwaka 2015.
Programu ya Kuimarisha Halmashauri (ULGSP) ambayo itafanyika katika miji 18 kwa lengo la kuziimarisha Halmashauri katika maeneo Makuu Matano ili ziweze kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi kwa kuzingatia Sera ya Ugatuaji wa Madaraka(D&D) ambayo OWM-TAMISEMI inatekeleza.
Maeneo yanayolengwa katika mradi huu ni masuala ya (i) Uboreshaji wa Mfumo wa Mipango miji, (iii) ukusanyaji wa mapato ya ndani hususani mapato yatokanayo na kodi ya majengo, (iii) uboreshaji wa mifumo ya udhibiti fedha na manunuzi pamoja na masuala ya mazingira na kijamii, (iv) uboreshaji wa mifumo ya utekelezaji, uendeshaji na utunzaji wa miundombinu kwa ajili ya huduma ya jamii pamoja na (v) uboreshaji wa uwajibikaji na uwazi.
Mradi huu unafadhiliwa na Benki ya Dunia kwa kiasi cha Dola za Kimarekani 255 na utatekelezwa katika Halmashauri za Miji 18 ya Tanzania Bara ambayo ni Iringa, Moshi, Tabora, Lindi, Babati, Kibaha,Singida, Njombe, Mpanda, Sumbawanga, Geita, Mpanda, Bariadi, Sumbawanga, Njombe, Musoma, Korogwe na Bukoba. Programu hii ilizinduliwa na Mhe. Waziri Mkuu tarehe 18 Juni Mwaka huu wa 2013 ambapo utekelezaji wake umeanza mwezi Julai, 2013 kwa kila Halmashauri kutangaza zabuni kwa ajili ya usanifu wa miradi itakayotekelezwa.
Ufanisi wa programu hii utavutia wadau wengine kushirikiana na Halmashauri nchini katika kutekeleza miradi mingine ya maendeleo.Pia itawezesha watakaotembelea Tanzania katika siku zijazo kupata faraja na huduma bora. Programu hii pamoja na miradi mingine inayotekelezwa itasaidia kubadilisha sura ya miji ya Tanzania kwa kuifanya ivutie kwa uwekezaji, kuishi na kufanya kazi.
Akizindua programu hii mjini Moshi hivi karibuni, Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Peter Pinda alizitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa zinajenga tabia ya kutenga bajeti kwa ajili ya kutunza miradi yote inayoanzishwa katika maeneo yao. Jambo ambalo linaendelea kusisizwa na OWM-TAMISEMI.
Benki ya Dunia imeiteua Tanzania kuwa nchi ya kwanza Barani Afrika kutekeleza Programu hii kama mradi wa mfano na majaribio ambapo katika utekelezaji wake mfumo wa kupima matokeo ya utekelezaji wa mradi ( Perfomance for Results) Utatumika.
Mradi huo utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano, kuanzia mwaka 2013 hadi 2018 kwa mkataba kati ya Benki ya Dunia na Serikali ya Tanzania, uliosainiwa mwezi Desemba mwaka 2012 ambapo jumla ya Dola za kimarekani milioni 255 zimetengwa. Dola milioni 201 kati ya hizo zitapelekwa moja kwa moja kwenye halmashauri na fedha zinazobakia zitatumika katika suala zima la kujenga uwezo wa halmashauri kwa kutekeleza mradi, pamoja na ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa programu.
IMETOLEWA NA OFISI YA WAZIRI MKUU
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top