Baadhi
ya wafanyakazi wa Tazara wakiwa nje ya ofisi ya mwajiri
WAFANYAKAZI
wa Shirika la Reli ya TAZARA Mkoani Mbeya wameingia katika Mgomo kwa muda
usiojulikana wakishinikiza Uongozi wa Shirika hilo kuwalipa mishahara yao ya
Miezi mine(4).
Aidha
watumishi hao wapatao zaidi ya 400 pia wamemwomba Waziri Mkuu Mizengo Pinda
kuingilia mgogoro huo kwa kile walichodai kuwa Ahadi ya Waziri wa Uchukuzi, Dk.
Harrison Mwakyembe aliyoitoa Agosti 3, Mwaka huu alipozungumza na wafanyakazi
kuwa ameshindwa kuitekeleza.
Wakizungumza
na waandishi wa Habari katika Ofisi za Tazara zilizopo Iyunga Jijini Mbeya baada
ya Maandamano yaliyoishia katika Ofisi ya Mwajiri walisema Shirika hilo
limeshindwa kuwalipa mishahara tangu Mwezi May Mwaka huu na kusababisha
Wafanyakazi kuishi maisha ya tabu.
Walisema
madai yao yameanza muda mrefu hali iliyopelekea Waziri Mwakyembe kufika na
kuzungumza nao na kuahidi kuwa Ifikapo Agost 22, Mwaka huu Menejimenti iwe
imelipa mishahara ya watumishi wote ikiwa ni pamoja na kukusanya madeni ya
wateja wao yanayofikia Bilion 5.
Walisema
hadi sasa hakuna kilichotekelezwa hali iliyowalazimu kugoma kujishughulisha na
kazi yoyote inayohusu Tazara hadi hapo watakapolipwa Mishahara yao au Waziri
Mkuu atakapoingilia na kutatua madai yao.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wafanyakazi wa Tazara kanda ya Mbeya (TRAWU), Christopher Kazio,
alisema hali ya wafanyakazi ni mbaya na inasababisha kuyumbisha usalama wa eneo
husika kutokana na baadhi yao kufukuzwa katika nyumba walizopanga kutokana na
ukosefu wa fedha.
Alisema
hali ya usalama nayo si shwari kutokana na wafanyakazi kuanza kuiba baadhi ya
vitu ili kujipatia chochote ili waweze kumudu ugumu wa maisha unaotokana na
ukosefu wa fedha kwa zaidi ya miezi minne ambayo wafanyakazi wnalidai
shirika.
Naye
Mwenyekiti wa wafanyakazi wa Tazara Mbeya Mjini Rafael Kazyoba, alisema
Wafanyakazi wote kwa ujumla wamekubaliana kutofanya kazi yoyote hadi hapo
uongozi wa Tazara utakapoamua kuwalipa mishahara yao na sio kutoa ahadi ambazo
wameshindwa kuzitekeleza.
Aidha
kwa upande wa kampuni ya ulinzi inayolinda katika Stesheni ya Mbeya ya Kilumi
Security nayo ikaibuka na kudai kuwa uongozi wa Tazara haujali maslahi ya watu
na kutekeleza mikataba inayotakiwa na kwamba wao kama walinzi wanapata wakati
mgumu wa kulinda usalama wa wafanyakazi walio na njaa wakiwemo wao
wenyewe.
Jemsi
Malembeka ni Afisa Rasilimali watu wa Kampuni hiyo ambaye alisema tangu waingie
Mkataba wa kulinda maeneo ya Tazara takribani Miezi 6 imepita hawajawahi kulipwa
hali inayosababisha walinzi kukimbia na wengine kujihusisha na wizi wa vitu vya
Tazara.
Wakati
madai ya wafanyakazi yakiendelea na huku wakitangaza mgomo mengine mapya
yakaibuka baada ya Wazee wastaafu na wajane wa Tazara kukjitokeza na kudai kuwa
tangu wastaafu kazi miaka ya 1993 Hadi 2003 hawajalipwa mafao
yao.
Juvenary
Ngaiza (mstaafu) na Aida Mbunda(Mjane) walisema tangu kustaafu kwao Serikali,
Tazara na mashirika ya Pensheni yameshindwa kulipa stahiki zao kwa muda mrefu na
wamekuwa hawatoi majibu ya kueleweka.
Walisema
ni vema mashirika hayo yakathamini mchango walioutoa wakiwa wafanyakazi wao na
siyo kuwasahau baada ya kustaafu hali inayowapekea kunyanyaswa pindi wakianza
kudai mafao yao ambayo ni haki yao.
Na
Mbeya yetu
|
Post a Comment