Mkuu
wa Kitengo cha Uhusiano na Huduma kwa Wateja kutoka Shirika la Taifa la
Hifadhi ya Jamii Bi. Eunice Chiume KUSHOTO akieleza kwa waandishi wa
habari kuhusu Mpango wa Shirika hilo kukusanya mapato ya shilingi
Bilioni 706.41 kutoka kwenye michango ya wanachama, wakati wa mkutano
uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam KULIA ni Mkurugenzi Msaidizi Idara
ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa.
PICHA NA ELIPHACE MARWA-MAELEZO
SHIRIKA LA TAIFA LA HIFADHI YA JAMII (NSSF)
TAARIFA KWA UMMA
Shirika
la Taifa la Hifadhi ya Jamii katika mwaka huu wa fedha linatarajia
kukusanya mapato ya Tshs. Billion 706.41 kutoka kwenye michango ya
wanachama ambao hadi mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu shirika lilikua
na wanachama 522,763 kwa nchi nzima.
Taarifa
iliyotolewa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya jamii kwa waandishi wa
habari imeeleza kwamba kiasi hicho cha michango kitatokana na
uandikishaji wa wanachama 169,241 wa mpango wa lazima na wanachama
85,158 wanaojiunga na NSSF kwa njia ya hiari.Katika kipindi hicho
waajiri 3,062 wanatarajia kuandikishwa kwenye Shirika kuungana na
waajiri 19,231 wa sasa na kufanya ongezeko la asilimia 84.07%.
Taarifa
pia imeeleza kuwa kiasi cha mafao kitakacholipwa ni shilingi bilioni
199 kwa wanachama watakaoacha au kustaafu kazi katika mwaka huu wa
fedha.
Katika mwaka huu wa fedha kiasi cha Tshs.bilioni 5.19 kitalipwa kwa ajili ya mafao ya matibabu kwa wanachama 254,399.
Wakati
huo huo katika mwaka huu wa fedha,shirika linatarajia kuwekeza kiasi
cha Tshs. Bilioni 951.4 ukilinganisha na Tshs bilioni 751.4 ambazo
ziliwekezwa katika mwaka wa fedha wa 2012/2013 sawa na ongezeko la
aslimia 21.06%.
Shirika
linatarajia pia kukusanya mapato ya Tshs.bilioni 181.1 kutoka kwenye
vitega uchumi ukilinganisha na mapato ya Tshs bilioni 120.1
zilizokusanywa mwaka jana wa fedha.
Maeneo ya uwekezaji ni pamoja na
ujenzi wa daraja la Kigamboni,Dhamana za serikali,mabenki,Ubia(Listed
&unlisted companies) na ujenzi wa nyumba za kuishi na biashara.
Tathmini
ya thamani ya mfuko wa shirika mwaka jana ilikua Tshs.Trilioni 2.1 na
thamani inatarajiwa kuongezeka na kufikia Tshs.Trilioni 2.6 katika
mwaka huu wa fedha ambapo ni sawa na ongezeko la asilimia 19.23%.
WIKI YA NSSF
Shirika
limeendelea kuadhimisha wiki ya NSSF kila mwaka kwa kushiriki katika
shughuli za kijamii kwa kuendesha michuano ya vyombo vya habari ambapo
michezo hiyo imetimiza mwaka wa 10 tangu ianzishwe mwaka 2004.
Mashindano
hayo ambayo yameanzishwa kwa madhumuni ya kujenga mahusiano kati ya
Shirika na vyombo vya habari mwaka huu yameshirikisha timu 17 za mpira
wa miguu na pete ambazo zilicheza mwezi machi mwaka huu kwa muda wa wiki
mbili.
Timu
hizo ni NSSF yenyewe kama mdhamini, TBC, New Habari Corporation,
Mwananchi, Habari Zanzibar, IPP Media,Sahara Communications, Radio
Kheri, Free Media, Business Times, Uhuru/Mzalendo, Global Publishers,
Tumaini Media, Changamoto, TSN, Mlimani Media na Jambo Leo.
Katika mashindano ya mwaka huu mabingwa kwa upande wa mpira wa miguu ni timu ya Jambo Leo na mpira wa pete ni Business Times.
TAARIFA HII IMETOLEWA NA SHIRIKA LA TAIFA LA HIFADHI YA JAMII (NSSF), AUGUST 21, 2013
Post a Comment