Mwanariadha akiajiandaa kukimbia mbio fupi za mita 100 uwanja wa jamhuri Morogoro. PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
indano hayo.
PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
Mita 400.
Morogoro.
Mashindano ya Riadha ya Taifa, yameanza kutimua vumbi leo kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini hapa huku zaidi ya wanariadha 450 wakitarajiwa kuchuana kuwania medali.
Mashindano ya Riadha ya Taifa, yameanza kutimua vumbi leo kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini hapa huku zaidi ya wanariadha 450 wakitarajiwa kuchuana kuwania medali.
Tayari wanariadha kutoka mikoa mbalimbali wameshawasili mjini hapa.
Mashindano hayo yamekuwa alama ya
maandalizi kwa ajili ya kusaka vipaji vya kushiriki mashindano ya
kimataifa, kama Jumuiya ya Madola mwakani, na yale ya Afrika ya vijana
mwaka huu nchini Maurtius.
Makocha wa timu shiriki walitambiana, huku kila mmoja akijinadi kutwaa medali.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti muda mfupi baada
ya kuwasili mjini Morogoro, makocha hao kila mmoja alidai timu yake
kutwaa ubingwa.
“Vijana wako fiti na bahati nzuri tuna wanariadha
wa michezo ya miruko, mitupo na mbio. Natoa tahadhari kwa mikoa mingine
wajiandae kupokea vichapo,” alitamba kocha wa Pwani, Robert Kalyahe.
Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Dar es Salaam,
Zainabu Mbiro alisema kuwa mkoa wake umejipanga vizuri kutwaa medali
kibao kwenye mashindano hayo.
Rais wa Chama cha Riadha Tanzania, Anthony Mtaka alisema maandalizi yote yamekamilika na mbio zitaanza saa 2:30 asubuhi.
CREDIT: JUMA MTANDA BLOG
Post a Comment