Mjumbe
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Prof. Palamaga mbaKabudi (wapili
kulia|) akizungumza na Viongozi wa Mkoa wa Pwani leo Ijumaa (Agosti 2.
2013) wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe. Halima Kiemba
(kushoto), Katibu Tawala wa Mkoa, Bi. Bertha Swai (wa pili kushoto).
Wajumbe wa Tume walifika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya
kupokea taarifa za maandalizi ya Mikutano ya Mabaraza ya Katiba katika
Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mkoani humo, kulia ni Mjumbe wa Tume,
Mhe. Al-shaymaa Kwegyir.
Mjumbe
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya Katiba, Profesa Palamaga mbaKabudi
akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya
Kibaha Mkoa wa Pwani wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika leo
(Ijumaa Agosti 2, 2013) katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya
Kilangalanga iliyopo Wilaya ni humo
Mjumbe
wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani,
Bi. Fediria Swai akichangia hoja kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya
iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya katiba katika mkutano uliofanyika
leo (Ijumaa Agosti 3, 2013) katika ukumbi wa Shule ya Sekondari
Kilangalanga iliyopo Wilayani humo.
Wajumbe
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Palamaga mbaKabudi (kushoto),
Al- Shaymaa Kwegyir (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi
wa Mkoa wa Pwani wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mhe. Halima
Kiemba (wa pili kulia) na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Bi. Bertha Swai
mara baada ya Wajumbe wa Tume kupokea taarifa ya Maandalizi ya Mikutano
ya Mabaraza ya Katiba katika Halmashauri za Wilaya na Miji ya Kibaha.
(PICHA NA TUME YA KATIBA)
Post a Comment