TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
1.
Hivi karibuni tumepata uhakika kuwa Tanzania Premier League (TPL) na
Azam Media wanayo nia ya kuingia mkataba wa kuonyesha mechi za Ligi Kuu
(Premier League) kwa msimu wa 2013/2014, 2014/2015 na 2015/2016
2.
Baada ya Kamati ya Utendaji ya YANGA kufanya uchambuzi wa kina juu ya
taarifa ya makubaliano ya kibiashara ya TPL / Azam Media ilihitimisha
kuwamkataba huu hauna maslahi kwa YANGA, na kwa hivyo, Kamati ya
Utendaji ya YANGA ilifikia uamuzi kuwa mechi za YANGAzisirushwe hewani
na Azam Media.
Mkutano Agosti 18; Yussuf
Manji ameitisha Mkutano Yanga
kuijadili Azam Media
Kwa
kuwa wawazi, Kamati ya Utendaji ya YANGA ilitoa taarifa kwa wanachama
wa YANGA kupitia vyombo vya habari tarehe 29 Julai, 2013 ambapo iliweka
bayana sababu zake na kueleza kuwa YANGAhaina tatizo na vilabu vingine
vya mpira wa miguu ikiruhusu mechi zao kurushwa na Azam Television ila
haifurahii kuwa TPL inalazimisha YANGA kuonyesha mechi zake za Vodacom
Premier League katika Azam Television.
Sote
tumeona baada ya hapo kuwa “nguvu ya ziada” inatumika kupotosha msimamo
wa Kamati ya Utendaji ya YANGA na kuidhalilisha Klabu ya YANGA
hadharani.
Juu
ya hayo Na Kwa kushangaza Sana, baadhi ya vilabu vya mpira WA miguu
ambavyo vina sifa kuwa havijawahi kushinda Ligi Kuu, vimeundwa hivi juzi
tu, havina uzoefu wowote WA kucheza soka kimataifa n.k. vina kuja
kuyapanga Kamati ya Utendaji ya YANGA jinsi ya kuendesha shughuli za
Klabu ya Yanga, vikiwa vinasahau vilabu vyao wenyewe na badala yake
kuiingilia YANGA kwa sababu zinazojionyesha wazi.
Inadhihirika
wazi kwamba kuna ushirikiano usio mzuri unaoashiria kula njama
kuilazimisha YANGA iruhusu mechi zake zirushwe na Azam Television.
Kwa
kuwa YANGA ni Klabu ya Wanachama yenye kupata nguvu kutokana na misingi
yake ya kidemokrasia iliyojijengea na uamuzi wake wa mwisho unatokana
na Wanachama wake mwenyewe, umeamua kuliweka suala hili zima kwa
Wanachama wa Yanga ili waamue ni njia gani ya kufuata kwa maslahi ya
Klabu yetu.
Kwa
kuzingatia hali hiyo basi, na kulingana na mamlaka niliyonayo kama
Mwenyekiti wa YANGA, natangaza mkutano wa dharura wa Wanachama wa YANGA
tarehe 18 Agosti, 2013 utakaofanyika uwanja wa Sabasaba kwenye ukumbi wa
PTA saa 3.30 asubuhi waje tujadiliane na kuamua suala la Azam
Television kurusha mechi za YANGA.
(YUSUF MANJI)
MWENYEKITI WA YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB
Manji ameitisha Mkutano Yanga
kuijadili Azam Media
Post a Comment