Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MUUAJI MPYA WA COASTAL YAYO LUTIMBA APOKEWA KIFALME TANGA

 

Na Oscar Asenga, Tanga,
MAPOKEZI wa Mshambuliaji Mpya wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga aliyetokea timu ya Mamlaka ya Mapato nchini Uganda (URA),Yayo Lutimba  kwenye uwanja wa Ndege Mkoani Tanga jana yalikuwa ya aina yake kutokana na kulakiwa na wingi wa mashabiki,viongozi na wanachama wa timu hiyo.
Mapokezi hayo yalianza saa mbili asubuhi na mchezaji huyo kutua saa nne katika uwanja wa ndege akiwa na Meneja wa timu hiyo Akida Machai ambaye alikuwa ameambatana naye kutoka nchini Uganda.


Mshambuliaji wa Mpya wa klabu ya Coastal Union ya Tanga Yayo Lutimba akitoka uwanja wa Ndege wa Tanga mara baada ya kutua akitokea nchini Uganda kushoto kwake ni Meneja wa timu ya Coastal Union Akida Machai ambaye alimfuata nchini humo.
Awali aliripotiwa katika gazeti la Uganda New Vision la jana (juzi) liliripoti kuwa mchezaji huyo alisajiliwa na Yanga ya Tanzania.
Akizungumza katika mapokezi hayo,Katibu wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga,Kassim Eli Siagi alisema wameingia mkataba wa miaka miwili na mchezaji huyo ambaye ataitumia timu hiyo kuanza msimu mpya wa ligi kuu utakaoanza Agosti 24 mwaka huu.
El Siagi alisema kuwepo kwa mchezaji huyo katika kikosi kuteleta chachu na upinzani mkubwa na hivyo kuipa mafanikio timu hiyo.


Katibu Mkuu wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga, Kassim El Siagi kulia mwenye shati la mistari meupe katikati ni Mshambuliaji huyo Yayo Lutimba  na kulia ni shabiki wa timu hiyo  Miraji Wandi.
Awali akizungumza mara baada ya kuwasili uwanjani hapo,Lutimba alihaidia kucheza kwa kujituma ili kuweza kuipa mafanikio timu hiyo pamoja na kushirikiana na wachezaji wenzake ili kutimiza malengo yao.
CREDIT: BIN ZUBEIRY BLOG
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top