Mkuu
wa Jeshi la Polisi IGP Said Mwema akiongea na Wanamichezo wa Polisi
Tanzania wanaoshiriki Michezo ya nane ya Majeshi ya Polisi kwa Nchi za
Kusini mwa Afrika (SARPCCO GAMES) nchini Namibia wakati alipowatembelea
katika hoteli waliyofikia katika jiji la Windhoek.(Picha na Frank
Geofray-Jeshi la Polisi, Windhoek Namibia)
Mkuu
wa Jeshi la Polisi IGP Said Mwema akiwasalimia Wanamichezo wa Polisi
Tanzania wanaoshiriki Michezo ya nane ya Majeshi ya Polisi kwa Nchi za
Kusini mwa Afrika (SARPCCO GAMES) nchini Namibia wakati wa ufunguzi wa
Michezo hiyo katika uwanja wa Taifa wa Namibia.(Picha na Frank
Geofray-Jeshi la Polisi, Windhoek Namibia)
Baadhi
ya Wanamichezo wanaounda timu ya Polisi Tanzania inayoshiriki michezo
ya nane ya Majeshi ya Polisi kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO
GAMES) nchini Namibia wakiwa katika picha ya pamoja moja wakati wa
ufunguzi wa michezo hiyo katika uwanja wa Taifa wa Namibia. (Picha na
Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Windhoek Namibia)
Kikundi
cha Sarakasi kikitoa burudani wakati wa ufunguzi wa Michezo ya nane ya
Majeshi ya Polisi kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO GAMES) nchini
Namibia katika uwanja wa Taifa wa Namibia.(Picha na Frank Geofray-Jeshi
la Polisi, Windhoek Namibia)
Wanamichezo
wa Polisi Tanzania wanaoshiriki Michezo ya Majeshi ya Polisi kwa Nchi
za Kusini mwa Afrika (SARPCCO GAMES) nchini Namibia wakipita mbele ya
mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa Michezo hiyo katika uwanja wa Taifa wa
Namibia.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Windhoek Namibia)
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Windhoek Namibia.
Hatimaye
michezo ya nane kwa majeshi ya Polisi kusini mwa Afrika (SARPCCO GAMES)
yamefunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Namibia Dk Hage Geingob katika
uwanja wa Taifa wa Namibia na kupambwa na burudani mbalimbali zikiwemo
ngoma, nyimbo sarakasi na maonyesho ya helkopta.
Ufunguzi
wa mashindano hayo ulihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo Wakuu
wa Majeshi ya Polisi kutoka nchi wanachama wa SARPCCO akiwemo IGP Said
Mwema.
Akizungumza
katika ufunguzi huo Dk Geingob alizitaka timu zinazoshiriki mashindano
hayo kushindana kwa nidhamu na kudumisha urafiki uliopo ili kuweza
kukabiliana na uhalifu kwa kubadilishana mbinu na mikakati kutoka katika
mataifa yao kwa lengo la kuwa na ukanda salama wa Kusini mwa Afrika.
Alisema
nchi zinashiriki zinahitaji ushindi lakini ni vyema zikatambua kuwa
timu moja na bora ndiyo itakayonyakua ushindi kwa kuwa mshindi ni mmoja
tu kati ya mataifa yote yaliyoshiriki.
Wakati
huohuo Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Said Mwema amewataka
wachezaji wa Tanzania kuhakikisha kuwa wanarejea na ushindi ili kupata
zawadi nono ambazo amewaaandalia endapo wataibuka na ushindi katika
michezo hiyo.
IGP
Mwema aliyasema hayo wakati alipowatembelea na kuzungumza na wachezaji
wa Tanzania katika hoteli waliyofikia ili kuwapa hamasa na morali
wakati wote wa michezo hiyo.
Alisema
kitu kikubwa ambacho wachezaji hao wamekifuata nchini Namibia ni
ushindi hivyo wahakikishe kuwa wanacheza michezo yote kwa morali na
kuibuka na ushindi jambo ambalo litalitea taifa na Jeshi la
Polisi sifa.
Post a Comment