Abainika kuzificha kwenye `laptop`
Kutupwa jela miaka 40
Kutupwa jela miaka 40
Makubi ambaye amepandishwa kizimbani
kujibu mashtaka, aliweka dawa hizo kwenye laptop mbovu, iliyokamatwa
muda mfupi baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Los Angeles,
akitokea Nairobi nchini Kenya.
Kwa mujibu wa taarifa za Shirika la
Habari la The Associated Press (AP) na San Jose Mercury News-California
(yote ya Marekani) zilizochapishwa kwenye mtandao, Makubi alikutwa
na heroine yenye uzito wa gramu 800.
AP ilikariri taarifa za shirika la habari
la City News Service, likiandika kuwa Makubi, aliyefikishwa katika
Mahakama ya Jimbo la Los Angeles, Jumatano wiki hii, alikiri kosa la
kufanya biashara hiyo nchini Marekani.
Kufuatia kukiri huko, Makubi anatarajiwa
kupewa hukumu ya kifungo cha miaka 40 jela na sasa yuko rumande
akisubiri kuanza kifungo chake Septemba Mosi mwaka huu, kwa mujibu wa
sheria za Marekani.
AP ilikariri taarifa za Mkaguzi wa Idara
ya Forodha ya uwanja wa ndege wa Los Angeles, zikieleza kuwa laptop ya
Makubi ilikuwa nzito `kupindukia wakati ilipopekuliwa.
“Tulijaribu kuiwasha lakini haikuwaka na
kubaini kuwa ilikuwa imeharibika, tulipofunguliwa tulibaini kuna gramu
800 za heroine,” mtandao huo ulikariri chanzo cha taarifa hiyo.
Makubi aliwaambia maofisa wa uwanja huo
kuwa alitoka Nairobi, Kenya na alikwenda Los Angeles akiwa njiani
kuelekea Alabama kukutana na mwanamke aliyekuwa anawasiliana naye
kupitia mtandao wa ‘internet’.
Matukio ya Watanzania kukamatwa na dawa za
kulevya yanatisha kutokana na wengi kunaswa na mihadarati sehemu
nyingi duniani ikiwamo China, Pakistan, Hong Kong , Kenya na Afrika
Kusini.
Pia Tanzania inatajwa kuwa na idadi kubwa
ya wafungwa kwenye magereza ya ughaibuni, waliopatikana na hatia za
kusafirisha dawa hizo kwa kubeba tumboni au kuzisafirisha kwa kutumia
mbinu nyingine.
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam, sasa unaelezwa kuwa ni kitovu cha kupitisha dawa hizo.
CHANZO:
NIPASHE JUMAPILI
Post a Comment