Mwenyekiti
wa Kampuni za IPP, Dk. Reginald Mengi akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa
shindano la wazo bora juu ya kujikwamua kiuchumi ‘Kutweets na Mengi’, Tony
Alfred katika hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
Washindi
wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Dk. Reginald
Mengi.
Hongera kwa
kushika nafasi ya kwanza.
DAR ES
SALAAM, Tanzania
MWENYEKITI
wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi,amesema vijana wanaosubiri mifumo iliyowekwa
iwasaidie kujikwamua kiuchumi wataendelea kubaki kuwa watumwa wa maamuzi ya watu
wengine.
Mengi
alitoa kauli hiyo jijini Dar esSalaam, leo wakati akikabidhi zawadi kwa washindi
watatu walioshinda shindano la wazo bora la 'kutweets na Mengi'.
Amesema kwa
sasa vijana wengi wanamaliza elimu ya msingi Sekondari na vyuo vikuu ambao
hawana ajira wala mitaji na wengi wao wanajisikia kama hawana pa
kutokea.
Aliongeza
kuwa licha ya serikali, jamii na wazazi kuwa na wajibu katika jambo hili kijana
anapaswa kuwa mtu wa kwanza kutafuta njia inayowezekana kwake.
Swali la
mwezi julai lililowatoa washindi hao liliuliza “Kijana asiyekuwa na ajira wala
fedha anawezaje kuanza kujijenga kiuchumi”ambapo Tony Alfred muuza kahawa katika
kituo cha mabsi Ubungo aliibuka mshindi wa kwanza.
Alfred
ambaye ni msomi wa shahada ya masoko kutoka chuo kikuu cha Da resSalaam,
aliwashinda John Mkungu na Maduhu Jumanne kwa jibu lake lililoeleza kuwa “kama
kijana fikiria katika hali uliyopo ni nini unachoweza kufanyia jamii yako,
ukipata jibu huo ndio mtaji na ajira yako.”
Kutokana na
ushindi huo Alfred amejipatia Sh Mil 1 ambapo John Mkungu alishika nafasi ya
pili na kujipatia kiasi cha Sh laki 5 na maduhu jumanne alijipatia sh. laki
3
Mengi
aliongeza kuwa kutokana na watu wengi kuchangia katika mtandao wake wa kijamii
wa Tweeter, ataanda mpango wa kuyakusanya mawazo yaliyokuwa mazuri na kuyaweka
katika mfumo sahihi kisha kuyafikisha kwa vijana wengine kupitia mashuleni na
vyuoni.
Akizungumzia
ushindi wake Alfred alisema Alfred alimshukuru Mengi kuanzisha mfumo huo na
kuwataka vijana wenzake wasikate tamaa pale wanapokosa ajira za
serikali.
Post a Comment