Na
Bryceson Mathias
ASKARI
Polisi (pichani) mwenye namba D5788D Koplo Patrice Masiko wa Upelelezi Wilaya ya
Dodoma, amemwandikia Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akipinga
kufukuzwa kwa aibu Juni 24, 2011.
Katika
barua yake ya Agosti 2, mwaka huu, Masiko anamuomba Makamu wa Rais Dk. Bilal,
amsaidie kumhimiza Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Said Mwema, ampe Majibu ya
rufaa ya Mashitaka ya Kijeshi yaliyosikilizwa tangu Novemba 30, 2010 hadi Juni
24, 2011.
Katika
barua hiyo kwa Dk. Bilal, Masiko anasema, anamuombi amsaidie kumhimiza IGP
ampatie majibu ya rufaa ya Mashitaka na Hukumu ya Kijeshi dhidi yake,
yaliyosikilizwa na ZM Majunja na SSP-OCD Mpwapwa toka Novemba 30, 2010 hadi Juni
24, 2011.
“Julai 19,
nilimwandikia IGP rufaa ya kupinga mwenendo mzima wa Mashitaka na Hukumu
iliyotolewa lakini sikupata majibu. Agosti 16, 2011 nilimwandikia tena
kukumbushia, lakini sijapata majibu.
“Tangu hapo
mpaka leo sipati mshahara wala Posho kitendo ambacho ni Uonevu, Ukatili,
Unyanyaswaji, na pia ni kinyume cha Sheria” ilisema sehemu ya barua hiyo ambayo
gazeti hili linacho Kivuli chake.
Aidha
Masiko ameorodhesha sababu Nane zilizopelekea kukata rufaa, ikiwemo kunyimwa
nakala ya mashitaka kwa ajili ya utetezi, kutozingatiwa kwa PGO, 104 (4), PGO
106 (28) (C), Kukosa Imani na Msikilizaji, kutojulishwa tarehe ya Kesi,
kutotendewa haki PGO 106 (24), kutopewa nafasi ya kujitetea na kuita mashahidi,
kesi kuhukumiwa mkewe akiumwa, Mkutano wa Kizota 2010, na ushahidi wa
PHQ.
Post a Comment