Mwnamuziki
mkongwe wa muziki wa dansi wa bendi ya Msondo Ngoma, Mzee Muhidin
Gurumo, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uamuzi wake wa
kustaafu rasmi kazi ya muziki aliyoifanya kwa muda wa miaka 53 sasa.
Gurumo alitoa kauli hiyo leo katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo
jijini Dar es Salaam. Picha na Magreth Kinabo.
************************************
Na Jennifer Chamila, Maelezo.
MWANAMUZIKI
mkongwe wa bendi ya Msondo Ngoma Mzee Muhidin Gurumo amestaafu rasimi
kazi ya muzika alioifanya kwa muda wa miaka 53.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mzee Gurumo mwenye
umri wa miaka 73 amesema ameamua kustaafu kazi hiyo kwa hiari yake
mwenyewe kutokana na umri wake kuwa mkubwa.
“Muziki
kwangu umekuwa kama asili yangu na kazi yangu lakini nimeamua kustaafu
kutokana na umri wangu na nitabaki kuwa mshauri tu kwa mwanamuziki
yeyote atakayetaka ushauri wangu,”alisema Mzee Gurumo.
Pamoja
na kufanya kazi ya muziki Gurumo alisema kuwa hakupata mafanikio
makubwa zaidi ya kujenga nyumba anayoishi na familia yake.
“Mimi nimeimba
kwa muda mrefu sana lakini hata baiskeli sina,”alisema Mzee Ngurumo.
Hata hivyo alisema nashukuru kuwa ana nyumba ya kuishi na familia.
Vilevile
Mzee Gurumo amewaasa vijana kuwa wabunifu na kuupenda mziki wa zamani
kwani ndio chimbuko la bongofleva na kuwashauri wanamuziki wa sasa kuwa
wavumilivu kukaa muda mrefu kwenye bendi moja ili hata wanapoondoka
mchango wao uthaminiwe.
Mzee Gurumo ambaye
ana mke na watoto wanne alisema kuwa katika maisha yake ya muziki
alifanikiwa kutunga nyimbo 60,000 na anavutiwa zaidi na mwanamziki
Hussein Jumbe na Hassani Lehan Bichuka na kwa wanamuziki wa kizazi kipya
anavutiwa na Nassibu Abdul ’Diamond’.
Mwanamuziki
huyo mkongwe alianza kufahamika katika tasnia ya muziki wa dansi kwenye
miaka ya 1960 ambapo mwaka 1964 alikuwa miongoni mwa waanzilishi wa
bendi ya Nuta Jazz na Mlimani Park.
Alidumu
na Mlimani Park mpaka mwaka 1985 na kuhamia Safari Sound aliyofanya
nayo kazi mpaka mwaka 1990 na kujiunga na Msondo Ngoma mpaka sasa
alipoamua kutangaza rasmi kustaafu kazi hiyo ya Kimuziki.
Post a Comment