Robert Mugabe anaapiswa leo kuwa rais wa Zimbabwe kwa awamu ya saba mfululizo.
Siku
hii ya leo ya Alhamisi imrtangazwa kuwa siku ya mapumziko nchini humo
ili kuwapa nafasi wafuasi wanaomuunga mkono rais huyo mwenye miaka 89
kuhudhuria sherehe za kuapishwa zinazofanyika katika uwanja mkubwa wa
michezo mjini Harare.
Sherehe
hizo za kuapishwa zilikuwa zikicheleweshwa na pingamizi mahakamani
lilifunguliwa na mpinzani wake mkubwa Morgan Tsvangirai kwa madai ya
kuwa uchaguzi uligubikwa na udanganyifu.
Hata
hivyo mahakama ya katiba ilitumbilia mbali kesi hiyo, na kutangaza kuwa
kuchaguliwa kwa Mugabe kulikuwa kwa huru na kwa haki.
Mugabe alipata asilimia 61 ya kura za urais dhidi ya asilimi 34 za Tsvangira katika uchaguzi wa Julai 31 mwaka huu.
Uchaguzi
huo umemaliza serikali ya kugawana madaraka iliyoundwa na viongozi hao
wawili mwaka 2009, chini ya shinikizo la viongozi wa Ukanda wa Afrika,
kufuatia uchaguzi uliokuwa umefanyika mwaka mmoja kabla kugubikwa na
vurugu na madai ya wizi wa kura.
Waziri Mkuu wa zamani na Kiongozi wa Upinzani Tsvangira amesema hatahudhuria sherehe hizo za kuapishwa.

Wakato huo huo Rais wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete na ujumbe wake wako mjini Harare kuhudhuria sherehe hizo zinazofuatia ushindi wa Rais Mugabe na chama chake cha ZANU-PF katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika nchini humo Julai 31, mwaka huu.
Post a Comment