KATIBU wa
NEC, Itikadi na Uenezi, CCM, Nape Nnauye amesema japokuwa mabadiliko ni
muhimu kwa maisha ya binadamu lakini lazima kila yanapohitajika
yafanywe kwa umakini mkubwa ili yasiwe na madhara.
hdg
Amesema
ni kutokana na sababu hiyo, ndiyo maana CCM imekuwa ikisisitiza umakini
na busara kubwa vitumike wakati huu ambao Tanzania ipo katika mchakato
wa kupata katiba mpya.
Nape
amesema miongoni mwa mambo ambayo CCM inaona kwamba lazima yatazamwe kwa
umakini na busara kubwa kabla ya hatua ya mwisho, ni kuhusu Tanzania
kuwa na serikali ngapi, ambapo rasimu ya kwanza ya Katiba inapendekeza
serikali tatu.
Nape
ambaye alikuwa akizungumza wakati akifungua Kongamano la Vijana mkoani
Mwanza lililofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu (BOT)
Kapripoint jijini Mwanza, juzi, alisema, kwa upande wake CCM kuhusu
kipengele hicho cha Tanzania kuwa na serikali ngapi, msimamo wake ni
serikali mbili.
"Sisi CCM
tunapotangaza msimamo wetu kwamba nchi hii inastahili kuwa ya serikali
mbili, haina maana kwamba tunadharau au kuwaona wapuuzi wanaopendekeza
ziwe tatu, la, msimamo wetu huu tunaueleza kwa hoja ili hatimaye jamii
ya Watanzania ikiziona zina mantiki watuunge mkono", alisema Nape.
Aidha
Nape alisema, umuhimu wa kuwa makini na kutumia busara katika jamii
kuhitaji mabadiliko unatokana na kwamba jamii ikiyapokea kwa pupa
huambulia yasichotarajia, ikiwemo machafuko au uongozi wasiohitaji kwa
ajili ya kukidhi matakwa yao ya maendeleo.
Nape
alisema katika pupa ya kutafuta mabadiliko, zipo baadhi ya nchi kama
Misri ambazo hadi sasa zimekosa utulivu kutokana na kupokea vibaya dhana
ya mabadiliko, wakaingia mitaani lakini bila kuchukua tahadhari,
hatimaye wamejikuta mabadiliko waliyopata nayo hawayataki tena, wanataka
mengine.
Akifafanua
alisema, CCM inatambua kwamba, muundo wa serikali mbili ndio utafaa
katika kudumisha Muungano, kuliko serikali tatu ambazo CCM inaona kwamba
mbali ya kuwa mzigo zaidi kwa wananchi, pia ni kuongeza changamoto juu
za zile zilizopo sasa kwenye muungano.
Post a Comment