Katibu mkuu wa shirikisho la soka Tanzania, Angetile Osiah
********
Na Boniface Wambura, TFF
Timu
ya 3Pillars Football Club ya Nigeria sasa inaruhusiwa kucheza mechi za
kirafiki nchini baada ya kupata idhini ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
la Nigeria (NFF).
Awali
tuliikatalia timu hiyo kucheza mechi za kirafiki nchini kwa vile
haikuwa na barua kutoka NFF, lakini sasa Shirikisho hilo limetoa idhini
hiyo. Pia ziara yake haikuwa inaratibiwa na wakala wa mechi
anayetambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) au
mwanachama wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Klabu
hiyo kutoka Jimbo la Lagos ilipanga ziara hiyo kwa kuwasiliana na chama
cha mpira wa miguu cha jimbo hilo ambacho nacho kilitakiwa kuomba
idhini NFF kwa niaba ya 3Pillars.
Hivyo
timu hiyo inaweza kucheza mechi, kwani ziara hiyo sasa inaratibiwa na
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) ambaye ni
mwanachama wetu.
Tunapenda
kukumbusha kuwa watu pekee wanaotakiwa kuandaa mechi za kirafiki za
kimataifa ni mawakala wa mechi wanaotambuliwa na FIFA au wanachama wa
TFF.
Post a Comment