Mratibu
wa mradi wa kujitolea wa Wafanye Watabasamu, Katunisti Nathan Mpangala
‘Kijasti’ (mwenye kijibegi mgongoni), akisaidiana na familia, ndugu,
jamaa na marafiki kuteremsha zawadi kwa ajili ya watoto wanaoumwa
saratani, Jumamosi iliyopita, Hospitali ya Taifa Muhimbili. Karibu na
‘Kijasti’ kulia ni ‘Mama Kijasti’.
Baadhi
ya watoto wanaotibiwa saratani, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es
Salaam, wakionesha uhodari wa kuchora wakati walipotembelewa na mradi wa
Wafanye Watabasamu, unaoratibiwa na Nathan Mpangala, Jumamosi
iliyopita. Watoto hao wapatao 80, walizawadiwa sabuni za kuogea/kufulia,
dawa za meno, biskuti, toilet papers, mafuta ya kupakaa, matunda na
vifaa mbalimbali vya kuchorea toka kwa marafiki wa mradi huo. Zaidi
bofya; https://www.facebook.com/pages/Wafanye-Watabasamu-Make-Them-Smile/140812046112398
Wachora
vibonzo, Nathan Mpangala ‘Mtukwao’ wa ITV, (kulia) na Abdul King O
‘Kaboka Mchizi’ wa Nipashe, wakichora na malaika wanaoendelea na
matibabu ya saratani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es
Salaam, Jumamosi iliyopita, wakati wa ziara ya mradi wa Wafanye
Watabasamu, hospitalini hapo. Mengi kuhusu zoezi hili, tembelea; https://www.facebook.com/pages/Wafanye-Watabasamu-Make-Them-Smile/140812046112398 
Rafiki
wa Wafanye Watabasamu ambaye pia ni katunisti wa magazeti ya Mwananchi,
Masoud Junior, akishuhudia umahiri wa kuchora toka kwa baadhi ya watoto
wanaoendelea na matibabu ya saratani katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili, Dar es Salaam, juzi, wakati wa ziara ya mradi wa Wafanye
Watabasamu. 
Ilikuwa
jambo la kutia moyo kuona watoto hawa wanasahau maumivu ya saratani kwa
muda na kujikita kwenye uchoraji. Mratibu wa Wafanye Watabasamu, Nathan
Mpangala, anawashukuru wachoraji wenzake, ndugu na marafiki wote
waliochangia muda, sadaka na tabasamu kwa watoto hao.
Mkurugenzi
wa Mawasiliano wa Shirika lisilo la Kiserikali la SIKIKA, Bi. Lilian
Kallaghe, (kushoto), yeye aliamua kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa
kuungana na marafiki wa Wafanye Watabasamu, ili kuwafariji watoto
waoendelea na matibabu ya saratani katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili, Dar es Salaam, juzi.
Mratibu
wa Wafanye Watabsamu, Nathan Mpangala, akishuhudia vipaji vya uchoraji
toka kwa baadhi ya watoto wanaoendelea na matibabu ya saratani katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, Jumamosi iliyopita.
Matukio mbali mbali ya ziara hiyo. 
Malaika akionesha umahiri wa kuchora.
Post a Comment