Mwakilishi
wa Shiriki la NSSF kutoka Makao Makuu jijini Dar,Bwa.Salim Khalfan
akielezea fursa mbalimbali zinazopatikana kwa mtu yeyote anayejiunga na
shirika la NSSF,alifafanua hayo leo kwenye ukumbi wa Luluma,nje kidogo
ya mji wa Singida,Salim alibanisha kuwa mtu yeyote atakayejiunga na
shirika hilo atanufaika na mambo mengi,ikiwemo suala la matibabu,mikopo
na mengineyo lukuki yanayopatikana ndani ya shirika hilo.Semina
hiyo ambayo inafanyika ikiwa ni mkoa wa tatu huu,ikianzia Kigoma,Tabora
na sasa Singida,iliandaliwa na Clouds Media Group na kufadhiriwa na
shirika la NSSF,Zantel,MaxMalipo,Lake Oil.PICHA NA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM
Pichani
juu ni sehemu washiriki wa semina ya Fursa kwa vijana,wakifuatilia mada
mbalimbali zilizokuwa zikizungumzwa kwenye semina hiyo,ambayo
imeonekana kuwavutia vilivyo kwa sehemu ya wakazi wa mji wa Singida
waliojitokeza kushiriki.
Mkurugenzi
wa Vipindi na Uzalishaji kutoka Clouds Media Group,Ruge
Mutahaba,akizungumza mbele ya washiriki wa Semina ya Fursa ndani ya
ukumbi wa Luluma,nje
kidogo ya mji wa Singida, kuhusiana na fursa mbalimbali wanazozipata
vijana na kuhakikisha wanazitumia ipasavyo,aliongeza kuwa vijana wengi
wamekuwa ni watu wa kulalamika lalamika tu na kukata tamaa mapema,aidha
Ruge amewataka vijana kuwa na muamko wa kufanya kazi na kujituma kwa
bidii pale fursa yoyote inapotokea.
Mmoja
wa Watangazaji mahiri wa Clouds FM,Millard Ayo akizungumza mbele ya
vijana wenzake ,nama alivyobahatika kuzitumia fursa mbalimbali alizokuwa
akizipata kwa ufasaha na kwa umakini mkubwa mpaka hapo
alipo,anabainisha kuwa kilichompelekea hapo alipo mpaka sasa ni namna
alivyojijenga kwa nidhamu,kujituma na bidii kubwa ya kazi kila alipokuwa
akiipata fursa,aidha amewataka vijana wenzake kuacha tabia ya kukata
tamaa mapema na kutokuwa wavivu wa kufanya kazi,kwani kwa kufanya hivyo
maendeleo hayatapatikana kirahisi.
Post a Comment