Na Onesmo Ngowi, Rais wa IBF/Africa
Katikati
ya miaka ya 90, nchi ya Tanzania ilipata bahati ya kuwa na bingwa wa
ngumi wa dunia ambaye alitambuliwa na Umoja wa Ngumi wa Dunia (WBU).
Rashid Matumla aliweza kuonyesha dunia kwamba Tanzania pia inaweza
kushindana na kushinda katika medani ya ngumi za kulipwa hivyo aliweza
kujizolea sifa kemkem yeye binafsi pamoja na nchi yetu ya Tanzania.
Ilikuwa ni miaka ya msisimko kwenye ngumi za kulipwa na wadau pamoja na
mabondia wengi walisisimka na uwezekano wa nchi yetu kuweza kushinda
mataji mengi zaidi ya Afrika, Mabara pamoja na dunia.
Wakati
Rashidi akiwa bingwa wa dunia, mdogo wake Mbwana naye alikuwa bingwa wa
mabara alietambuliwa na WBU pia. Hiyo iliongeza chachu na hamasa kwa
wadau wa ngumi za kulipwa hivyo nchi ilikuwa kwenye shamrashamra za aina
ya pekee.
Mkuzaji
(Promota) aliyefanya mambo yote hayo si mwingine bali ni Kampuni ya DJB
Boxing Promotions iliyokuwa inamilikiwa na kuendeshwa kwa umahiri na
ndugu wawili Dionis Malinzi na Jamal Malinzi. Ndugu hawa wazalendo kweli
waliweza kuwekeza kiasi kikubwa sana katika kuwaendeleza kina Matumla
pamoja na mabondia wengine wengi hapa Tanzania. Ni Watanzania wachache
alioweza kushiriki au kuwekeza katika michezo kama kina Malinzi na hiyo
iliweza kuitangaza nchi yetu kwa kiasi kikubwa.
Kina
Malinzi hawakuwaandalia tu mapambano kina Matumla bali walienda mbali
na kuwapeleka nchini Afrika ya Kusini ili waweze kufanya mazoezi kwenye
gyms zilizokwa na vifaa vya kisasa pamoja na wataalamu mahiri
waliowafanyia mazoezi na kubadili kabisa uwezo wao wa kupigana kuwa wa
hali ya juu kama mabondia wezngie katika nchi zilizoendelea.
Tanzania
imepita katika kipindi kirefu na kigumu bika kuweza kuwa na msisimko
kama ule ambao kina Matumla chini ya kina Malinzi waliuleta nchini.
Pamoja na kwamba Magoma Shabani kutoka Tanga alikuja pia kuwa bingwa wa
dunia aliyetabuliwa pia na WBU lakini ule msisimko waliouleta kina
Matumla na kima Malinzi ulishafifia.
Ujio
wa bondia Francis Cheka na wengine wa jika lake umeanza tena kufufua
matumaini na msisimko wa ngumi za kulipwa hapa Tanzania. Cheka bondia
kutokaMorogoro ameweza kuwa kivutio pekee wa ngumi za kulipwa kwa sasa
hapa Tanzania na Afrika ya Mashariki kwa ujumla.
Francis Cheka ni bondia pekee katika bara la Afrika ambaye ameweza kushinda na kutetea taji la IBF kwa kipindi kirefu.
Nikiwa
kama Rais wa IBF katika bara la Afrika,Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya
Kati, ninaona faraja kubwa sana kuwa karibu na bondia Francis Cheka. Kwa
kweli umahiri wake sio tu kwenye ulingo bali ni namna Cheka
anavyojichanganya na watu wengine katika jamii.
Francis
Cheka anatambuliwa kuwa bondia namba 4 katika viwango vya mabara vya
IBF na ni bondia pekee katika bara la Afrika aliye na kiwango cha juu
kama hicho katika orodha ya mabondia wa kiafrika katika uzito wake wa
Super Middle.
Tanzania
imeona na kushughudia malumbano mengi katika ngumi za kulipwa ambayo
yanaletwa na sababu ambazo hazina msingi. Tumefikia mahali tumalize
tifauti zetu na kukaa meza moja ili tuweze kuuendeleza mchezo wa ngumi
za kulipwa hapa nchini kwa faida ya taifa letu ili kuwapata kima Matumla
na kina Cheka wengi zaidi. Pia ushirikiano wetu utawapa moyo kina Malinzi wengi zaidi kuweza kushirikiana katika kuuendeleza mchezo wa ngumi.
Nataka
itambulike rasmi kuwa bondia ana HAKI ya kuchagua ni taji lipi au chama
kipi anataka kupigania. Chaguo lake lisilete mzozo au vivu kati ya
wanaosimamia mchezo wa ngumi badala yake ulete ushirikiano utakaoweza
kumsaidia bondia mwenyewe ili aweze kushinda na kuitangaza nchi yetu
vizuri.
Ndiyo
maana naona faraja sana kwa bondia Francis Cheka kupata nafasi ya
kupigana pambano la dunia. Kwangu mimi Francis Cheka ni bingwa wangu wa
Afrika (IBF) mpaka atakapopanda ulingoni siku ya tarehe 30 Augusti
katika ukumbi ya Diamond Jubilee. Mimi
itakuwa mmoja wa maelfu ya Watanzania watakaokwenda katika ukumbi ule
kumshangilia Francis Cheka akiipeperusha bendera ya Tanzania.
Kwa
kawaida bingwa wa shirikisho moja akishaamua kuwania mkanda wa
shirikisho lingine anapoteza ubingwa wa shirikisho alilokuwa
analishikilia. Lakini nimechukua pia jukumu la kuhakikisha kuwa kwa
bahati mbaya kama Cheka akishindwa kuupata ubingwa wa dunia hatapoteza
ubingwa wake wa IBF Afrika. Pia hatapoteza viwangio vyake alivyonavyo
katika IBF. Hii itamsadia kuweza kung’ara zaidi.
Mimi
nadhani imefikia wakati sasa sisi watanzania wenye nia nzuri ya
maendeleo kushirikiana na kuhakikisha kuwa nchi hii inapiga hatua kwenye
medani ya ngumi.
Hongera Sana Francis Cheka pamoja na waandaaji wa mpambano huo muruwa.
Post a Comment