|
Picha ya pamoja |
|
Madereva
Bodaboda wakijipanga tayari kwa kwenda kupokea vyeti
vyao |
|
Madereva
Bodaboda wakiandamana kuelekea kupokea vyeti vyao toka kwa kamanda wa polisi
mkoa wa Mbeya |
|
Kamanda
wa wa Polisi Mkoani MBEYA DIWAN ATHUMAN akiongea na madereva Bodaboda kabla ya
kuwakabidhi vyeti vyao |
|
Madereva
walikabidhiwa vyeti hivyo baada ya kupatiwa mafunzo ya alama za usalama
barabarani kwa msaada wa shirika lisilo la Kiserikali kwa kushirikiana na Kikosi
cha usalama Barabarani Mkoani Mbeya. |
|
Picha
ya pamoja |
|
Kamanda
wa wa Polisi Mkoani MBEYA DIWAN ATHUMAN Ametoa vyeti kwa madereva wa pikipiki
maarufu kama Bodaboda zaidi ya 151 wa Igurusi Wilaya ya Mbarali.
Madereva
hao walikabidhiwa vyeti hivyo baada ya kupatiwa mafunzo ya alama za usalama
barabarani kwa msaada wa shirika lisilo la Kiserikali kwa kushirikiana na Kikosi
cha usalama Barabarani Mkoani Mbeya.
Mbali
ya kukabidhiwa vyeti pia Madereva hao walipatiwa leseni za udereva ambapo Diwani
Athumani aliwataka madereva hao kuwa makini barabarani na kuzingatia sheria za
usalama barabarani.
Aidha
Kamanda Diwani aliwashukuru madereva wa Bodaboda kwa ushirikiano na Jeshi la
Polisi kwa kufichua vitendo vya uhalifu Mkoani Mbeya ambapo wamekuwa wakitoa
taarifa za siri na kupunguza uhalifu mkoani Mbeya.
Hata
hivyo Diwani alitumia fursa hiyo kuwataka madereva kuwa makini kwani kwa kipindi
cha miezi sita madereva 38 wa bodaboda wamefariki mkoani Mbeya na kusikitishwa
na wingi wa ajali hizo za pikipiki kwani wengi wao ni vijana na ni nguvu kazi ya
Taifa.
Na
Mbeya yetu
|
on Friday, August 23, 2013
Post a Comment