Naibu
katibu Mkuu (UVCCM) Zanziba,Shaka Hamdu Shaka (kushoto) akiongea na
waandishi wa habari leo Agosti 21,2013 , Makao Makuu ya Umoja wa Vijana
(CCM) jijini Dar es salaam wakati akitoa pongezi kutoka Umoja wa Vijana
wa Chama cha mapinduzi(UVCCM) kutokana na hatua zilizochukuliwa na Rais
wa Zanziba Dk.Ali Mohamed Shein ambaye amefanya mabadiliko ya Baraza
lake la Mawaziri na kupangua Idara zilizokuwa zikisimamiwa na Wizara
mbalimbali (kulia) Mjumbe Kamati Teule (UVCCM) Taifa, Nadra Juma
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza kwa umakini Naibu katibu Mkuu (UVCCM) Tanzania Zanziba,Shaka Hamdu Shaka, leo Agosti 21,2013
PICHA NA PHILEMON SOLOMON FULLSHANGWE DAR ES SALAAM
Na Philemon Solomon wa Fullshangwe Dar es salaam
Naibu
katibu Mkuu UVCCM Zanzibar, Shaka Hamdu Shaka amesema Rais Dkt. Shein
ni msikivu, makini na hodari wa kusoma alama za nyakati na mabadiliko
yake, hivyo amefanya hayo kwa nia nzuri akilenga kuwatumikia wananchi
chini ya mfumo wa umoja wa kitaifa.
Ameongeza
kuwa UVCCM Zanzibar itashirikiana naye bega kwa bega katika kuhakikisha
kuwa anatimiza malengo ya serikali na ilani ya chama cha mapinduzi.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 53 cha Katiba ya
Zanzibar ya 1984 Jana amefanya marekebisho katika muundo na majukumu ya
baadhi ya Wizara za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kufuatia
marekebisho hayo, baadhi ya shughuli za Wizara zimeunganishwa na
kuundiwa Wizara mpya na baadhi zimehamishiwa katika wizara mpya na
baadhi zimehamishiwa katika wizara nyengine.
Hata hivyo marekebisho hayo hayakuongeza idadi ya Wizara na kwa hivyo zinaendelea kubaki wizara 16.
Post a Comment