Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe aataendelea
na awamu ya saba ya uongozi nchini humo baada ya Tume ya taifa hilo ya uchaguzi kumtangaza mshindi REUTERS/Philimon Bulawayo |
Na Martha Saranga
Amini
Hatimaye tume ya taifa ya uchaguzi nchini
Zimbabwe imetangaza matokeo ya urais na rais Robert Mugabe kuibuka mshindi kwa
asilimia 61.09 akifuatiwa na mpinzani wake waziri mkuu Morgan Tsvangirai,matokeo
ambayo yalikuwa yakisubiriwa kwa hamu na ulimwengu mzima.
Awali Waziri mkuu Tsvangirai alilalamikia
uchaguzi wa wabunge na uraisi kugubikwa na utata na kuahidi kuchukua hatua za
kisheria kupinga matokeo hayo.
Bwana Tsvangirai alidai kuwa chama chake cha
MDC hakitakuwa radhi kushirikiana na chama cha raisi Mugabe Zanu-PF.
Vyama hivyo vikuu vya siasa nchini Zimbabwe
vimekuwa katika mgogoro tangu mwaka 2009 baada ya uchaguzi mkuu uliopita ambapo
uligubikwa na ghasia.
Matokeo ya mwishoni mwa juma yalionesha chama
cha MDC kilibananishwa na kupata ushindi hafifu wa viti vya ubunge 49 wakati
chama cha raisi Mugabe Zanu-PF kkikijizolea jumla ya viti 158.
Via kiswahili.rfi.fr
Post a Comment