Balozi wa Malaria ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), Leodger Tenga akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kupiga vita
ugonjwa wa malaria iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Malaria ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), Leodger Tenga akipeana mkono na Meneja Kiongozi, Uhusiano Huduma kwa Wateja wa NSSF, Eunice Chiume wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kupiga vita
ugonjwa wa malaria iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Mafao ya Matibabu wa Shirika la Taifa
la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ali Mtulia akizungumza wakati wa hafla ya
uzinduzi wa kampeni ya kupiga vita ugonjwa wa malaria kwa kushirikiana na
Wizara ya Afya, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) pamoja na NSSF.
Msama Promotions kumwaga madawati Kinondoni
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI
ya Msama Promotions imejipanga kutoa madawati kwa shule mbalimbali za
msingi zilizoko Wilayani Kinondoni Jijini Dar es Salaam kabla ya mwaka
2014.
Akizungumza
na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita Mkurugenzi wa kampuni hiyo,
Alex Msama alisema ugawaji wa madawati hayo utakwenda sambamba na
ugawaji wa sare na vifaa mbalimbali vya shule.
Msama alisema hivi sasa ameunda kamati maalumu ya kutembelea shule ambazo zina upungufu wa madawati na vifaa vingine.
Msama Promotions ni kampuni ambayo imesaidia jamii kwa muda mrefu, ambapo sasa imeamua kujikita katika suala la elimu.
Alisema
mpaka sasa wameshatengeneza madawati yapatayo 50,000 na kwamba dhamira
ya kampuni hiyo ni kuinua kiwango cha elimu katika Jiji la Dar es
Salaam, ambapo kwa kuanzia wanaanzia katika wilaya ya Kinondoni.
“Kampuni
ya Msama promotions imedhamiria kuwasaidia waanafunzi wa shule za
msingi wasome kwenye mazingira mazuri ambayo yatafanikisha maendeleo
yao na nchi kwa ujumla” alisema Msama.
Aliongeza
kuwa ili kufanikisha mipango ya kusaidia elimu, hivi sasa kampuni hiyo
iko kwenye mchakato wa kupata hati kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha
kimataifa cha kulelea watoto yatima na wasiojiweza.
Kituo hicho kinatarajiwa kujengwa katika eneo walilopewa na Rais Jakaya Kikwete lililopo Pugu, jijini Dar es Salaam.
Post a Comment