Na Boniface Wambura
Jumla
ya wanamichezo 58 wamerusha fomu kuomba kuteuliwa kuwania nafasi
mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) na ule wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) utakaofanyika
Oktoba mwaka huu.
Kwa
upande wa TFF waliorejesha fomu kwa upande wa urais ni Athuman Jumanne
Nyamlani,Jamal Emil Malinzi, Omari Mussa Nkwarulo na Richard Rukambura.
Nafasi ya Makamu wa Rais wamejitokeza Imani Omari Madega, Nasib Ramadhan
na Walace Karia.
Walioomba
nafasi za ujumbe kuwakilisha kanda mbalimbali ni Abdallah Hussein
Mussa, Kaliro Samson, Jumbe Odessa Magati, Mugisha Mujwahuzi Galibona,
Vedastus Kalwizira Lufano, Samwel Nyalla, Epaphra Amana Swai, Mbasha
Matutu Mong’ateko, Stanslaus Haroon Nyongo, Ally Mtumwa, Elley Simon
Mbise na Omari Walii.
Ahmed
Msafiri Mgoyi, Yusuf Hamisi Kitumbo, Ayoub Nyaulingo, Blassy Kiondo,
Nazarius Kilungeja, Ayoub Shaib Nyenzi, Cyprian Charles Kuyava, David
Lugenge, Elias Mwanjala, Eliud Peter Mvela, John Mwachendang’ombe
Kiteve, James Patrick Mhagama, Kamwanga Rajabu Tambwe na Stanley William
Lugenge.
Athuman
Kambi, Francis Kumba Ndulane, Zafarani Damoder, Charles Komba, Hussein
Mwamba, Stewart Ernest Masima, Farid Salum Nahdi, Geoffrey Nyange,
Riziki Majala, Twahil Twaha Njoki, Davis Elisa Mosha na Khalid Abdallah
Mohamed.
Wengine
ni Alex Chrispine Kamuzelya, Juma Abbas Pinto, Muhsin Balhabou, Omar
Isack Abdulkadir, Shaffih Dauda Kajuna na Wilfred Mzigama Kidao.
Kwa upande wa uchaguzi wa TFF mwombaji ambaye hakurudisha fomu ni Venance Mwamoto pekee.
Kwa
upande wa TPL Board waliojitokeza kuwania uongozi wa juu ni wawili tu;
Hamad Yahya Juma (Mwenyekiti) na Said Muhamad Said (Makamu Mwenyekiti).
Walioomba
nafasi za ujumbe wa TPL Board ni Kazimoto Miraji Muzo, Michael
Njunwensi Kaijage, Omari Khatibu Mwindadi, Salum Seif Rupia na Silas
Masui Magunguma.
Post a Comment