SIKU chache baada ya Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini kudai jeraha alilonalo katika bega la kulia limetokana na risasi aliyopigwa na polisi mkoani Morogoro, baadhi ya Waislamu nchini wametoa tamko la kumtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ajiuzulu mara moja.
Msimamo huo umetolewa Dar es Salaam jana katika kongamano la
Waislamu ambalo lilifanyika katika Uwanja wa Mwembe
Yanga.Akizungumza katika kongamano hilo ambalo lilihudhuriwa
na mamia ya waumini wa dini hiyo, mmoja wa viongozi wa
jumuiya hiyo Shekhe Kondo Juma Bungo, alisema Waislamu
wanatoa muda kwa Dkt. Nchimbi kujiondoa katika nafasi hiyo
.
Alisema, mbali na Dkt. Nchimbi, walisema Kamanda wa Polisi
mkoani Morogoro, Faustine Shilogile, anapaswa kukamatwa na
kufikishwa mahakamani wakidai ndiye mhusika mkuu wa kupanga
mikakati ya kumdhuru Shekhe Ponda.“Askari aliyempiga risasi
Shekhe Ponda na Kamanda ambaye alisimamia suala zima la
uvamizi kwa kiongozi wetu, wote wanapaswa kuwajibishwa.
tunataka iundwe tume huru ya uchunguzi badala ya timu
iliyoundwa na polisi,” alisema.
Al i o n g e z a k uwa , kama maazimio hayo yatapuuzwa na
wahusika pamoja na Serikali kushindwa kuchukua hatua stahiki,
itakuwa mwanzo na mwisho wa historia ya Tanzania.
“Kitakachotokea baada ya hapo, Serikali itaona mwanzo tu
lakini haitajua mwisho wake...Waislamu nchi nzima
watafanyamaandamano, polisi wanategemea kupandishwa
vyeo au kupewa posho nyingi pale yanapotokea matatizo ya
Waislamu. “Kwa sasa hali inavyoonesha watapandishwa vyeo
kwa uchungu kwani Waislamu hatutakubali,” alisema Shekhe
Bungo na kusisitiza kuwa, Shekhe Ponda ana thamani kubwa sana
kwa Waislamu.
lakini haitajua mwisho wake...Waislamu nchi nzima
watafanyamaandamano, polisi wanategemea kupandishwa
vyeo au kupewa posho nyingi pale yanapotokea matatizo ya
Waislamu. “Kwa sasa hali inavyoonesha watapandishwa vyeo
kwa uchungu kwani Waislamu hatutakubali,” alisema Shekhe
Bungo na kusisitiza kuwa, Shekhe Ponda ana thamani kubwa sana
kwa Waislamu.
Shekhe Bungo alilihadharisha Jeshi la Polisi kuacha kuwatisha
Waislamu na kuongeza kuwa, Serikali isije kuwalaumu kwa
kitakachotokea kama madai yao hayatatekelezwa.
Aliwataka Waislamu popote walipo, kutoa adhabu palevion gozi au
wanachama wa Cha maChaMapinduzi (CCM),wanapoingia
misikitinina kufanya kampeni za kuomba wachaguliwe katika
uchaguzi ujao.
Tamko la CUF
Katika hatua nyingine,Chama cha Wananchi (CUF), kimelitaka
Jeshi la Polisi nchini,limuachie Shekhe Ponda aweze ku
endelea na matibabu katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa(M OI)
.
Chama hicho kimesema kitendo alichofanyiwa Shekhe Ponda cha
kuondolewa MOI wakati hali yake kiafya haijatengemaa,si cha
kibinadamu bali cha kinyama.
kibinadamu bali cha kinyama.
Mwenyekiti wa chama hicho Taifa,Profesa Ibrahim Lipumba,
aliyasema hayo Dar esS alaam jana wakati akizungumza na
waandishi wahabari.
"Kauli za vitisho na ubabe unaofanywa na Kamanda wa Polisi,
Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova,
vinachochea hasira na jazba za wananchi wengine wakiamini
kuwa, jeshi hilo lina lengo la kumuua Shekhe Ponda badala ya
polisi kujenga amani, wao wanaibomoa," alisema.
Prof. Lipumba alisema, jeshi hilo limeshindwa kufanya kazi kwa
weledi ndio sababu ya kuongezeka vitendo vya uhalifu na tuhuma
nyingi kwa baadhi ya polisi ambao wanashirikiana na wahalifu.
"Polisi wetu wameweka pembeni kazi yao ya kupambana na
uhalifu... wanapoteza wakati mwingi na raslimali
kumshughulikia Shekhe Ponda hivyo nawaomba Watanzania
wote tudai jeshi lenye weledi na linalowajibika," alisema.
kumshughulikia Shekhe Ponda hivyo nawaomba Watanzania
wote tudai jeshi lenye weledi na linalowajibika," alisema.
Alisema CUF kinaungana na Watanzania wote kulaani vikali
kitendo alichofanyiwa Shekhe Ponda, kumfungulia mashtaka na
kumuondoa MOI alipokuwa akipatiwa matibabu bila taarifa na
kumpeleka gerezani Segerea.
Aliongeza kuwa, jeshi hilo ndio chanzo cha wananchi kuvunja
amani ya nchi ambapo juzi mchana, alikwenda Segerea kumuona
Shekhe Ponda ambapo Mkuu wa gereza hilo alimpa ushirikiano
mzuri uliofanikisha amuone na kuzungumza naye.
" Ta y a r i S h e k h e P o n d a amepelekewa dawa zake gerezani
na amepewa huduma za tiba zinazoweza kupatikana katika gereza
hilo," alisema Prof. Lipumba na kuongeza kuwa, taarifa alizonazo
X-ray imeonesha risasi aliyopigwa imepita karibu na mfupa ambao
umepasuka.
Alisema hali ya Shekhe Ponda inaendelea vizuri ukilinganisha
na awali baada ya kufikishwa gerezani kwani anaweza
kutembea mwenyewe, anafahamu kamili na waliweza kutaniana
kutembea mwenyewe, anafahamu kamili na waliweza kutaniana
na mkuu wa gereza ambaye alimhakikishia kupata huduma nzuri.
Prof. Lipumba aliongeza kuwa, anazo taarifa kuwa Jeshi la Polisi
mkoani Morogoro linataka kumhoji daktari aliyemtibu Shekhe
Ponda, siku alipopigwa risasi.
"Inasikitisha kwamba polisi hawajapitia Taasisi ya Chama cha
Madaktari Tanzania (MAT), ili iombe kibali cha kufanya hivyo
badala yake wanataka kumsulubu daktari kwa kosa la kumtibu
Shekhe Ponda jambo ambalo linashangaza," alisema.
Aliongeza kuwa, CUF inataka Serikali iunde tume huru ambayo
itaongozwa na Jaji ili kuchunguza tukio la kupigwa risasi Shekhe
Ponda, askari aliyempiga na waliompa amri ya kufanya hivyo
wafikishwe mahakamani na kumfutia kesi ya uchochezi.
Shekhe Ponda alipata mkasa huu Agosti 10 mwaka huu mkoani Morogoro muda mchache baada ya kushiriki katika Kongamano la Baraza la Eid.
Post a Comment