Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Balozi
wa Jamuhuri ya Watu wa Kenya Nchini Tanzania Balozi Mutinda Mutiso hapo
Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwasilisha salamu za
pole kwa Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Balozi Mutinda Mutiso kufuatia
uwanja wa ndege wa Kimataifa wan chi hiyo kukum bwa na Moto. Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Aboud Mohammed.
Balozi
wa Kenya Nchini Tanzania Mutinda Mutiso akimkabidhi Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kamusi ya Kiingereza kwa Kiswahili
aliyoitunga kwa ajili ya kukuza lugha hiyo pamoja na kusaidia wana
diplomasia.
********************************************
Na Othman Khamis Ame
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar imetoa pole kwa Wananchi wa Jamuhuri ya Watu
wa Kenya kutokana na maafa ya moto mkubwa uliokikumba Kiwanja cha Ndege
cha Kimataifa cha Jomo Kenyata Kiliopo Mjini Nairobi Nchini humo na
kusababisha hasara kubwa ambayo bado haijajuilikana.
Moto
huo umesabisha safari zote za ndege zilizopangwa kuingia na kutoka
kwenye uwanja huo kusitishwa na kupelekea ndege hizo kutua katika
viwanja vyengine vya ndege vya Eldoret, Mombasa na Nchi jirani za Afrika
Mashariki.
Pole
hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi wakati alipofanya mazungumao na Balozi wa Kenya Nchini Tanzania
Balozi Mutinda Mutiso aliyefika kumuaga hapo Ofisini kwake Vuga Mjini
Zanzibar baada ya kumaliza muda wa utumishi wake wa miaka minne hapa
Nchini.
Balozi
Seif alisema Wananchi wa kenya wamekumbwa na maafa hayo yaliyosababisha
kutishia kutetereka kwa uchumi wake unaotegemea kwa kiasi kikubwa
huduma zinazotolewa na Uwanja huo katika ukanda mzima wa Bara la Afrika
ukiunganisha ndegembali mbali za Kimataifa.
Alisema
gharama za kuufanyia matengenezo uwanja huo ni kubwa kufuatia moto huo
uliotokea mapema alfajiri ya Jumatano katika eneo la kuwasili abiria
kabla ya kusambaa hadi maeneo mengine likiwemo lile la Idara ya
Uhamiaji.
Alifahamisha
kwamba umefika wakati kwa Waafrika kuwa makini na vitendo vya kuwatia
hofu wananchi { Ugaidi } ambavyo vinaweza kusababisha ukosefu wa utulivu
na amani miongoni mwa Jamii.
Alimueleza
Balozi Huyo wa Jamuhuri ya Watu wa Kenya Nchini Tanzania kwamba Vitendo
vya Kigaidi vinavyoonekana kujitokeza katika Nchi mbali mbali Duniani
vikilikumba pia Bara la Afrika humfanya Mtu aishi katika maisha ya hofu
na wasi wasi.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimpongeza Balozi huyo wa Kenya Nchini
Tanzania kwa juhudi zake za utumishi zilizochangia kuimarika zaidi kwa
uhusiano wa kudugu uliopo kati ya Kenya na Tanzania na Zanzibar kwa
ujumla.
Balozi
Seif alisema Wananchi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania hasa wale
wanaoishi katika ukanda wa Pwani ya Mwambao wa Afrika Mashariki wamekuwa
na uhusiano wa karibu na kidugu na wenzao wa Taifa la Kenya.
Alishauri
uhusiano huo ukazidi kuimarishwa kwa faida ya wananachi wa pande hizo
mbili hasa kwa kuzingatia zaidi muingiliano uliopo kupitia Jumuia ya
Afrika Mashariki iliyounganisha harakati za kiuchumi za mataifa
wanachama.
Mapema
Balozi wa Jamuhuri ya Watu wa Kenya Nchini Tanzania Balozi Mutinda
Mutiso alisema upo umuhimu wa wana Jumuiya ya Afrika Mashariki kuendelea
kuikuza na kuithamini Lugha ya Kiswahili kwa lengo la kuipa heshima
yake Kimataifa.
Balozi
Mutiso alisema inasikitisha kuona wenye Lugha ya Kiswahili wanaendelea
kusua sua wakati lugha yenyewe kimataifa inazungumzwa takriban na watu
zaidi ya Milioni mia mbili na arubaini duniani kote ikiwa lugha ya nne
kwa ukubwa duniani hivi sasa.
“
Takwimu za watu wanaozungumza Kiswahili Duniani ndizo zilizonishawishi
mimi kufikia uwamuzi wa kutunga Kamusi la Kingereza kwa Kiswahili
kupitia mfumo wa Kidiplomasia ili kutoa mchango wangu katika kukuza
lugha yetu ya Afrika Mashariki. Mchango wangu huu pia nimekusudia
uwasaidie wanadiplomasia wenzangu “. Alifafanua Balozi Mutinda.
Akizungumzia
mchakato wa Katiba Mpya ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambao hivi
sasa unapita katika hatua ya Rasimu ya Katiba hiyo Balozi Mutinda Mutiso
ameipongeza Tanzania kwa hatua yake hiyo yenye muelekeo wa kutandika
Demokrasia zaidi.
Balozi
Mutinda alisema Waafrika walio wengi wanatarajia kukiona kipindi cha
mpito cha kuelekea kwenye Katiba Mpya Nchini Tanzania kinakuwa kigezo
na mfano bora wa kuigwa na kuungwa mkono na Mataifa mbali mbali ya Bara
la Afrika.
Aliipongeza
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyoamua kufuata mfumo wa Umoja wa
Kitaifa ambao umeleta utulivu, amani na umoja miongoni mwa Wazanzibari
walio wengi baada ya mgongano wa mrefu wa kisiasa uliovikumba vyama
vikuu viwili vya kisiasa.
Balozi
Mutinda alisema inapendeza kuona Zanzibar hivi sasa imetulia kisiasa
kwa kuwa na mfumo huo wa Serikali ya pamoja unaofaa kupongezwa na kuigwa
na Mataifa mengine yanayotaka kuelekea kwenye demokrasia zaidi ndani na
nje ya Bara la Afrika.
Post a Comment