Mshambuliaji
wa Yanga ya jijini Dar es Salaam, Mrisho Ngasa, akichuana kuwania mpira
na mabeki wa 3Pillars ya Nigeria, wakati wa mchezo wa kirafiki wa
Kimataifa, baina ya timu hizo uliochezwa leo jioni kwenye Uwanja wa
Taifa Jijini. Katika mchezo huo Yanga imeibuka na ushindi kiduchu wa bao
1-0, lililofungwa na Hussein Javu, katika dakika ya 40.
Mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete (katikati) akijaribu kuwatoka mabeki wa 3Pillars, wakati wa mchezo huo.
Mfungaji
pekee wa bao la ushindi katika mchezo wa leo, aliyepeleka furaha kwa
Wanajangwani, Hussein Javu, akiwatoka mabeki wa 3Pillars, wakati wa
mchezo huo.
Benchi la Wana wa Jangwani, likiwa na Mastaa kibao........Picha zote kwa hisani ya Global Publishers
Katika mchezo wa leo, mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara Dar Young Africans, waliuanza mchezo huo kwa kasi huku wakisaka ushindi ili kuendeleza rekodi ya kutofungwa katika michezo ya kirafiki ya kujipima nguvu kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2013/2014, inayotarajia kuanza Agosti 24, ambapo Yanga itafungua dimba na Ashant Utd ya Ilala, pamoja na maandalizi ya mchezo wake wa Ngao ya Hisani dhidi ya Azam Fc, utakaopigwa wiki ijayo.
Yanga iliwaanzisha baadhi ya washambuliaji wake wapya Hussein Javu na Mrisho Ngassa waliojiunga na kikosi hicho msimu huu.
Yanga ilikosa nafasi za wazi za kufungua kupitia kwa washambuliaji hao ambao hawakuonekana kuwa makini katika umaliziaji wa mipira iliyokuwa ikiwafikia.
Naye David Luhende, alikosa bao katika dakika ya 34 kufuatia mpira alioupiga kuokelewa na mlinda mlango wa 3Pillars FC ambao ulitoka na kuwa kona ambayo haikuweza kuzaa matunda, huku awali Said Bahanuzi akikosa nafasi pia kama hiyo dakika ya 17 ya mchezo.
Alikuwa ni Kingo namba moja Tanzania, Athuman Idd 'Chuji', aliyetoa pasi nzuri ya mwisho kwa mshambuliaji, Hussein Javu aliyeweza kuipatia Yanga, bao hilo la ushindi.
Post a Comment