Na
Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UONGOZI
wa Boom FC umelishukuru Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa
kuipatia msaada wa Sh 5, 125, 000 kwa ajili ya uendeshaji wa timu hiyo katika
Ligi Daraja la Pili Mkoa wa Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa NSSF, Ramadhani Dau
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana, Katibu mkuu wa Boom FC, Duni Mibavu amesema fedha
hizo zitasaidia timu kufanya vizuri katika ligi na kuwapa morali wachezaji ili
kuhakikisha timu hiyo inacheza Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao.
“Tunawashukuru
wenzetu wa NSSF chini ya Mkurugenzi wake Dk. Ramadhan Dau kwa msaada mkubwa
walioutupatia, hii inaonyesha ni jinsi gani walivyoguswa na na kilio chetu na
kuamua kutusaidia ili tufanye vizuri,” alisema.
Duni
ameomba na mashirika mengine pamoja na makampuni mbalimbali nayo kuiga mfano wa
NSSF katika kuzisaidia timu za madaraja ya chini ili nazo zifanye vizuri.
Post a Comment