Na
Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UONGOZI
wa klabu ya Yanga, umesema mechi yao ya kirafiki ya Kimataifa dhidi ya Sport
Club Villa ya nchini Uganda ni muhimu kwa ajili ya kumpa kocha nafasi ya
kuangalia mapungufu yao kabla ya kuanza patashika ya Ligi ya Tanzania Bara
itakayoanza Agosti 24 mwaka huu.
Msemaji
wa Yanga, Baraka Kizuguto, pichani.
Mechi
hiyo inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka hapa nchini, imepangwa kuanza
kutimua vumbi saa 10 za jioni katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam,
ambapo wadau wao watajionea burudani ya aina yake.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto, alisema kocha
wao Ernest Brandit, atapata fursa ya kuangalia uwezo wa vijana wake kabla ya
michuano kuanza.
Alisema
kabla ya ligi hiyo kuanza, Yanga pia itaingia uwanjani Agosti 17 kucheza mechi
ya kuwania Ngao ya Hisani dhidi ya timu ya Azam FC,iliyoweka kambi nchini Afrika
Kusini.
“Ni
mechi kali ya kirafiki dhidi ya Sport Club ya Villa ya Uganda, huku kiingilio
cha chini kabisa kwenye mchezo huo kikiwa shilingi 5000 kwa mzunguuko ili kutoa
fursa kwa mashabiki kuingia kwa wingi zaidi.
“Tunaamini
kocha wetu pamoja na benchi lote la ufundi litapata fursa ya kushuhudia makali
na mapungufu ya wachezaji wao ili waone namna ya kuboresha kwa ajili ya kuleta
ushindi katika mechi zijazo,” alisema.
Yanga
tayari imejigamba kujiandaa kikamilifu kwa ajili ya kutetea taji lao ililotwaa
msimu uliopita kutoka kwa mtani wao wa jadi, Simba SC, huku nafasi ya pili
ikienda kwa Azam watakayokutana nayo kugombea ngao ya Hisani.
Post a Comment