Spika
wa Bunge Mhe. Anne Makinda leo amefungua rasmi mkutano wa siku tatu wa
Baraza la Katiba la Chama cha wabunge wanawake Tanzania (TWPG) mjini
Bagamoyo. Pichani, Spika
wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwa katika meza kuu na viongozi wa TWPG
pamoja na mtoa mada katika kikao cha Baraza hilo Spika Mstaafu Mhe. Pius
Msekwa.
Naibu Katibu Mkuu wa TWPG Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa akiwakaribisha wajumbe.
Katibu Mkuu wa TWPG ambaye pia ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Jasmine Kairuki (MB) akielezeaMuhtasari wa Baraza hilo, Malengo na Matokeo yanayotarajiwa kwa mgeni rasmi.
Mwenyekiti wa TWPG Mhe. Anna Abdallah (MB) akitoa neno la ukaribisho. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPO CHINI
Mkuu wa Mkoa wa pwani Mhe. Mwantumu Mahiza akimkaribisha mgeni rasmi kufungua Baraza la katiba kwa wabunge wanawake.
Mgeni Rasmi Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akifungua rasmi baraza la Katiba kwa wabunge wanawake mjini Bagamoyo.
Spika Mstaafu, Mhe. Pius Msekwa akiwakilisha mada kwa wabunge wanawake kuhusu yaliyomo Kwenye Rasimu ya Katiba.
Baadhi ya Wabunge wakifuatilia mada kwa makini.
Mhe.
Lediana Mg'ong'o akichangia maoni yake wakati wa kujadili rasimu ya
katiba kwenye baraza la katiba la wabunge wanawake (TWPG) lililofanyika
Bagamoyo.
Picha ya pamoja baada ya kufungwa kwa baraza hilo.
Post a Comment