Bingwa
wa riadha mita 1500 katika michezo ya Umoja wa wakuu wa Polisi kusini
mwa Afrika (SARPCCO) Basil John wa Tanzania (Katikati) akiwa na mshindi
wa pili Zimbabwe (kushoto) na mshindi wa tatu Namibia (Kulia) baada ya
kukabidhiwa medali zao.Michezo hiyo inaendelea katika jiji la Windhoek
Nchini Namibia. .(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Windhoek
Namibia)
Bingwa
wa mbio za mita 5000 1500 katika michezo ya Umoja wa wakuu wa Polisi
kusini mwa Afrika (SARPCCO) Fabian Nelson wa Tanzania (Katikati) akiimba
wimbo wa Taifa baada ya kukabidhiwa medali yake ya dhahabu akiwa na
mshindi wa pili Wilbrado Peter wa Tanzania (Kushoto) na Mshindi wa Tatu
Zimbabwe (Kushoto). Michezo hiyo inaendelea katika jiji la Windhoek
Nchini Namibia. (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Windhoek
Namibia) Wanariadha
wa Tanzania (Kulia) wakiwa na wenzao wa Zimbabwe na Namibia wakiwa
katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa medali zao kwa kuibuka na
ushindi wa tatu katika mbio za kupokezana vijiti katika michezo ya Umoja
wa wakuu wa Polisi kusini mwa Afrika (SARPCCO) inayoendelea nchini
Namibia. Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Windhoek Namibia)
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Windhoek Namibia.
Timu
ya mpira wa miguu ya Polisi Tanzania inayoshiriki michezo ya Umoja wa
wakuu wa Polisi kwa nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO) imeanza vibaya
baada ya kupoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya timu ngumu na bingwa
mtetezi Polisi Zambia baada ya kukubali kichapo cha mabao 2 -1 katika
mchezo uliochezwa jana usiku katika uwanja wa taifa wa Namibia.
Mabao
ya Zambia yalifungwa na mshambuliaji hatari wa timu hiyo Musukuma
Chipunga katika dakika ya 15 na 20 baada ya uzembe uliofanywa na safu
ya ulinzi wa timu ya Polisi Tanzania.
Bao
la Tanzania lilipatikana kipindi cha pili kwa njia ya mkwaju wa penati
baada ya kuangushwa kwa John Kanakamfumu katika eneo la hatari wakati
akipokea pasi iliyopigwa na Saimon Lezire.
Penati
hiyo iliwekwa kimiani na John Kanakamfumu baada ya kuachia shuti kali
lililomshinda kipa wa Zambia ambaye jana alikuwa mwiba kwa Polisi
Tanzania baada ya kuokoa mashuti yaliyokuwa yakipigwa na wachezaji wa
Tanzania.
Hata
hivyo kipindi cha kwanza Polisi Tanzania haikucheza vizuri hadi kipindi
cha pili baada ya kuingia kwa Delta Thomas, Madope Mwingira na John
Kanakamfumu ambao walionyesha uhai kwa timu ya Tanzania.
Katika Mechi nyingine ya kundi A, Polisi Zimbabwe ilishinda 2-1 dhidi ya Afrika kusini.
Wakati
huohuo Wanariadha wameendelea kuipatia Tanzania Medali baada ya kuibuka
mabingwa katika mbio za mita 5000, 1500 na washindi wa pili katika 5000
na kurusha tufe.
Waliopata
medali jana ni pamoja na Fabian Nelson 5000 (Dhahabu), Basil John 1500
(Dhahabu), Wilbardo Peter 5000 (Fedha),Mohamed Ibrahimu katika kurusha
tufe (Fedha) na Basil John tena (Shaba) katika mbio za vijiti.
Mpaka
sasa Polisi Tanzania ina medali tisa huku tatu zikiwa za Dhahabu,tatu
za fedha na tatu za Shaba huku ikijiamini kupata medali nyingine katika
michezo ya kurusha vishale (dats) mpira wa pete, mpira wa miguu na mbio
za nyika.
Post a Comment