Mwenyekiti wa TASO Kanda ya nyanda za juu Kusini Kepten mstaafu Nkoswe
Siku
chache zikiwa zimebaki ili kufikia kilele cha maadhimisho ya s
kumeibuka mgongano baina ya Chama cha wakulima (TASO)na serikali kuhusu
maadhimisho hayo yafanyike Agosti 7au 8, mwaka huu.
********
Mgongano
huo umekuja baada ya serikali kutaka maadhimisho hayo yafanyike
Agosti 7 mwaka huu huku chama cha wakulima kikiweka msimamo wake wa
kusherehekea maadhimisho hayo agosti, 8 mwaka huu .
Akizungumza
jijini Mbeya katika viwanja vya John Mwakangale Mwenyekiti wa Chama cha
wakulima (TASO) kanda ya nyanda za juu kusini,Kapten Mstaafu Noel
Nkoswe wakati wa majumuisho na waandishi wa habari baada ya kuibuka vuta
nikuvute na serikali kuhusu kilelele cha maadhimisho hayo ya
wakulima.
Kapten
Nkoswe amesema kuwa wao kama chama cha wakulima msimamo wao upo pale
pale wa sherehe hiyo ya wakulima kufanyika Agosti 8 mwaka huu kama
ilivyopangwa kila mwaka.
Amesema
Wakulima wao lazima l washerekee sikukuu yao kama kawaida hivyo
mpango wa kubadilisha tarehe haupo ambapo chama hicho kwa msimao wake
kitafanya tarehe 8 na zawadi za wakulima kutolewa agosti 8 kama
ilivyo pangwa.
Kapten mstaafu Nkoswe amesema mwenyekiti wa TASO taifa aliyemtaja kwa
jina moja amemwelekeza kuwa maadhimisho ya kilele cha sikukuu hiyo
yatafanyika kitaifa katika kanda ya kati Dodoma Agosti 7 mwaka huu
ambapo katika kanda zingine zitafanya kama kawaida Agosti 8 mwaka huu.
Hata
hivyo kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt.Christine Ishengoma
amesema kuwa wamepokea barua ya serikali inayotaarifu sherehe za kilele
cha nane nane zifanyike Agosti 7 mwaka huu kutokana na sikukuu ya Idd
kuwa agosti 8 mwaka huu .
Hata
hivyo katika barua iliyotumwa na wizara ya kilimo chakula na ushirika
yenye kumbu kumbu namba AE 18/196/01 ya julai 30 mwaka huu kwenda kwa
waziri wa nchi sera uratibu na bunge ofisi ya waziri mkuu iliyoandikwa
na waziri wa kilimo na chakula Eng Christopher Chiza na nakala kwa
wakuu wa mikoa yote minne ya kanda ya nyanda za juu kusini.
Aidha
nakala ya barua hyo iliyotumwa kwa katibu mtendaji Taifa imesema kuwa
sherehe za kilele cha nane nane imeamliwa zifanyike Agosti 7 mwaka
huu kutokana na mwingiliano wa sikukuu ya Idd ambapo Waziri wa nchi
Mh.William Lukuvi atakuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo.
NA mbeya Yetu Blog
Post a Comment