Katika
gazeti la Nipashe la leo Jumatatu tarehe 5 Agosti, 2013 toleo Namba
057834 ukurasa wa mbele na wa nne kuna habari inayosomeka "Elimu: Aibu,
aibu". Katika habari hii mwandishi anaelezea kwamba kuna Madudu zaidi
yamebainika katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, baada ya
kuwapanga baadhi ya wanafunzi wa kidato cha tano kwenye shule ambazo
hazina masomo ya michepuo yao.
Habari
hiyo imenukuliwa kimakosa kutoka katika Tovuti ya Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi ambapo imepotosha ukweli wa Taarifa husika. Usahihi wa
Taarifa yenyewe ni kwamba wanafunzi waliobadilishiwa shule ni wale
walioomba wenyewe kubadilishiwa michepuo (combination) na si kwamba
walibadilishwa kutokana na kukosa michepuo waliyopangiwa awali katika
shule hizo.
Aidha,
wanafunzi wengine waliobadilishiwa shule ni wale waliopangwa mbali
kutoka sehemu wanazoishi, walio wagonjwa wanaohitaji kuwa karibu na
hospitali na walioomba kupangwa katika shule za kutwa kutokana na sababu
za kiuchumi.
Wizara
huwapanga wanafunzi wa Kidato cha tano kwa kufuata Taarifa zilizojazwa
na wanafunzi wenyewe kwenye Selection Form (SEL Form) ambapo wanafunzi
wanajaza machaguo yao kulingana na matarajio yao.
Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilitangaza matokeo ya kupangwa Kidato cha 5
wanafunzi waliohitimu kidato cha 4 mwaka 2012 tarehe 10 Julai, 2013.
Baada ya tangazo hilo, Wizara ilipokea maombi ya wanafunzi wanaotaka
kubadili shule au machaguo (combinations) walizopangwa kwa sababu
mbalimbali. Wizara ilitafakari maombi hayo na kufanya mabadiliko ya
shule/ machaguo.
Imetolewa na:
Ntambi Bunyazu
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Post a Comment