Naibu
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Benedict Nangoro akitoa
hotuba wakati wa uzinduzi rasmi wa Mashindano ya Mifugo Kitaifa leo
Agosti 05, 2013 katika Viwanja vya Maonesho ya Nane Nane, Nzuguni
Dodoma(Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
…………………..
Na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza, Dodoma
Naibu
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Benedict Nangoro
amaewataka Wafugaji nchini kuondokana na ufugaji wa Mifugo unaozingatia
wingi wa Mifugo kuliko kuzingatia uzalishaji.
Mhe.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ameyasema hayo leo wakati
wa Mashindano Maalum ya Mifugo Kitaifa yaliyofanyika katika Viwanja vya
Maonesho ya Nane Nane, Nzuguni Dodoma ambapo Taasisi mbalimbali za
Serikali, Mashirika na Wafugaji Binafsi wameshiriki Mashindano hayo.
Mhe.
Nangoro amesema kuwa lengo kubwa la Mashindano hayo ya Mifugo ni kutoa
fursa kwa Wafugaji hapa nchini kujifunza mbinu mpya na bora zaidi za
uzalishaji na uvunaji wa mazao ya Mifugo hivyo kuleta tija katika Sekta
ya Ufugaji wa Mifugo hapa nchini.
“Nawaombeni
sana ndugu zangu Wakulima na Wafugaji tujifunze njia hizo mpya na bora
za uzalishaji wa mazao ya Mifugo na Mwanafunzi mzuri ni yule anayeelewa
na kupata maarifa zaidi na kuyatekeleza katika utendaji wake wa kila
siku”. Alisisitiza Mhe. Nangoro
Aliongeza
kuwa Asilimia 80 ya Watanzania hapa Nchini katika Idadi yao ni Wakulima
na Wafugaji hivyo wakipatiwa Elimu ya Teknolojia na mbinu mpya za
uzalishaji na uvunaji wa mazao ya Mifugo Watanzania kujikwamua Kiuchumi
hivyo kupunguza umasikini hapa nchini.
Kwa
upande wake Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi,
Dkt. Yohana Budeba amesema kuwa Mashindano hayo ya Mifugo Kitaifa
yalizinduliwa rasmi mwaka 2011 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda kufuatia Agizo alilolitoa Mhe. Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa
Kilele cha Maonesho ya Nane Nane Kitaifa yaliyofanyika katika Viwanja
vya Nzuguni, Dodoma mwaka 2010 ili kutoa fursa kwa Wakulima na Wafugaji
kupata elimu na mbinu mpya za ufugaji wa Mifugo.
Dkt.
Budeba ameahidi kuwa Wizara yake itaendelea kushirikiana na Wafugaji
katika kuboresha Sekta ya Mifugo hapa nchini kwa kuwapatia huduma
muhimu za Mifugo ikiwemo upatikanaji wa pembejeo za Mifugo pamoja na
kushirikiana na Wadau Wengine ili kuboresha Soko la Mazao ya Mifugo hapa
nchini.
Mashindano
haya ya Mifugo Kitaifa yanafanyika kwa mara ya tatu ambapo mara ya
kwanza yalifanyika mwaka 2011 katika Viwanja vya Maonesho ya Nane Nane
Nzuguni, Mkoani Dodoma na washiriki mbalimbali hushiriki Mashindano haya
zikiwemo Taasisi za Serikali, Mashirika na Wafugaji Binafsi kwa lengo
la kutoa elimu ya umma kwa Wafugaji na mbinu bora za uzalishaji na
uvunaji wa mazao ya Mifugo.
Post a Comment