Kamishna wa Polisi
Kanda Maalum Dar es Salaam Suleiman Kova (kushoto).
Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda Maalum ya
Dar es Salaam kimeendesha operesheni mbalimbali za kukamata madereva na
waendesha pikipiki (bodaboda) wasiotii sheria na kanuni za usalama
barabarani.
Kufanyika kwa operesheni hiyo ni katika
kuhakikisha kwamba sheria na kanuni za usalama barabarani zinasimamiwa na
kufuatwa kikamilifu kwa nia ya kupunguza wimbi la ajali za barabarani.
Akitoa taarifa ya Kikosi cha usalama barabarani
kanda maalum Dar es Salaam, Kamishna wa polisi kanda maalum Dar es Salaaam
Suleiman Kova amesema kwa kipindi cha kuanzia tarehe 14 hadi 20. 08.2013 kikosi
hicho kimekamata magari 1,388, makosa 2,272 na pikipiki 884 na jumla ya wapanda
pikipiki 7 wamefikishwa mahakamani.
Amesema makosa yaliyolipiwa faini kwa
‘notification’ ni 2,260 ambapo jumla ya fedha zilizopatikana ni Shilingi
67,800,000/=.
Aidha amesema Operesheni hiyo inaendelea.
Chanzo MOBLOG
Post a Comment