MAANDAMANO ya amani
yaliyokuwa yameandaliwa na chama cha demokrasia na maendeleo(chadema) yamegeuka
shubiri kwa wakazi wa jiji la Mwanza baada ya kuibuka mapambano makali baina ya
waandamanaji hao na jeshi la polisi mkoani Mwanza na kusababisha polisi kutumia
nguvu kuwatawanya wafuasi wa chama hicho.
Maandamano hayo ya amani
ambayo yalianzia katika eneo la Buzuruga nje kidogo ya jiji la Mwanza yalikuw
ayakiongozwa na wabunge Highness Kiwia wa Ilemela pamoja na Ezekiel
Wenje kuelekea katika viwanja vya Furahisha yalilenga kumshinikiza Mkuu wa Mkoa
wa Mwanza Ernest Ndikilo kutoa barua zinazodaiwa kuandikwa na ofisi ya Waziri
Mkuu Tamisemi kuwarejesha madiwani watatu waliotimuliwa katika Manispaa ya
Ilemela kutokana na kushindwa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo.
Polisi wenye silaha
pamoja na askari kanzu walianza kutanda katika eneo hilo la Furahisha
wakiongozwa na Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai Mkoa wa Mwanza RCO Konyo
ambaye alikuwa akitumia gari lenye namba za usajili DK 068EXV aina ya Toyota
Land Cruiser
Maandamano hayo ambayo
awali yalionekana kana kwamba yangelimalizika salama yaliwasili katika viwanja
vya Furahisha majira ya saa 5.38 huku yakiongozwa na gari la polisi lenye namba
za usajili za nchi ya Uganda 779 UAG likiwa nimesheheni polisi wenye
silaha nzito ikiwa ni pamoja na mabomu ya machozi na bunduki pamoja na askari
kadhaa ambao walikuwa katikati ya maandamano hayo.
Baada ya maandamano hayo
kuwasili katika viwanja vya Furahisha kwa amani,waandamani hao ambao walikuwa
na mabango mbalimbali yaliyosomeka kuwa ‘Matata hatutaki uendelee kuwa Meya wa
Ilemela rudia kazi yako ya awali, na jingine Jaji Sumari tumechoka kuahirisha
mara kw amara kesi dhidi ya Matata na jingine lililosomeka kuwa RD
Ndikilo tunahitaji barua za kurejeshwa kwa madiwani wetu.
Hata hivyo tofauti na
ilivyokuwa imetangazwa kuwa maandamano hayo ya amani yangelipokelewa na Mkuu wa
Mkoa wa Mwanza Ernest Ndikilo,hakukuwa na kiongozi yoyote wa Serikali ambaye
alikuwepo uwanjani hapo kupokea maandamano hayo.
Kufuatia kutoonekana kwa
kiongozi yoyote wa Serikali,viongozi wa chadema pamoja na wabunge wao
walikutana kwa faragha kwa dakika kadhaa kwa ajili ya kujua hatima ya
maandamano hayo ambapo Mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje alipanda jukwaani saa
6.45 na kuwaeleza maelfu ya waandamanaji kuwa wameamua kumtuma Mbunge wa
Ilemela Highnes Kiwia kwenda ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kuchukua majibu
kwa ajili ya kuwaletea wananchi walioandamana juu ya hatima ya madiwani hao.
Hata hivyo saa moja
baadae Mbunge huyo alisimama jukwani na wakuwaeleza waandamani hao kuwa simu ya
Mbunge Kiwia ilikuwa haipatikani hivyo kuwataka kuandamana kwenda kwa Mkuu wa
mkoa wa Mwanza kujua kulikoni na hapo ndipo hali ya hewa ilipochafuka.
Jeshi la polisi baada ya
kuona wandamanaji hao wameanza kuelekea katika ofisi za Mkuu wa mkoa liliwataka
kutawanyika ambapo waandamanaji hao walikaidi ndipo jeshi la polisi lilipoamua
kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi hao.
Vurugu hizo ambazo
zilianza majira ya saa 7.30 zilisababisha kufungwa kwa baadhi ya barabara
kutokana na waandamanji hao kuweka vizuizi vya mawe na kuchoma matairi,ambapo
pia maduka na ofisi mbalimbali zililazimika kufungwa kwa muda kupisha vurugu
hizo.
Baadhi ya wananchi ambao
walikuwa wakitumia usafiri wa umma walionekana wakishuka kupitia katika
madirisha ya magari hayo na kukimbia kwa hofu ya kujeruhiwa na mabomu pamoja na
mawe ambayo yalikuwa yakirushwa na waandamanji hao kwa jeshi la polisi.
MKUU WA MKOA WA MWANZA
ALONGA.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza
akizungumza na Mbunge Kiwia pamoja na viongozi wa chadema ofisini kwake alisema
kuwa ameshangazwa na uvumi huo kuwa ofisi yake imekalia barua a kurejeshwa kwa
madiwani Abubakar Kapera(Nyamanoro),Dan Kahungu(Kirumba) pamoja na Marietha
Chenyenge(Ilemela).
RC Ndikilo alisema kuwa
Serikali imekuwa ikifanya kazi zake kwa maandishi na sio kwa kufuata maneno ya
mtaani na kueleza kuwa hana barua yoyote toka ofisi ya Waziri Mkuu inayomualifu
kuhusu kuwarejesha madiwani hao baada ya kukata rufaa.
“Hata Mbunge kuna siku
ulinipigia simu ukiniuliza juu ya kuwepo kwa barua hizo name nilikujibu kuwa
kwa kuwa uko hapo Bungeni Dodoma ambapo pia kuna ofisi ya Waziri Mkuu
nilikujibu kuwa ni muhimu ukawaona viongozi wakuu wa Tamisemi ikiwa ni pamoja
na Waziri Mkuu,pia nilikushauri kuwa wakupe japo nakala ya barua hiyo”,alisema
RC Ndikilo.
“Lakini cha kushangaza
nimekuwa nikisikia maneno ya ajabu kuwa nimeficha barua za madiwani
hao,ikumbukwe kuwa madiwnai hao hawakukata rufaa kwangu bali walikata rufaa
ngazi ya juu kabisa,ili kukata mzizi wa fitina naomba kati ya tarehe 26 hadi 27
wewe Mbunge pamoja na mimi twende TAMISEMI kukutana na viongozi ili kukata
mzizi wa fitina na tuje tuwaeleze wananchi ukweli uliopo”,alisema RC Ndikilo.
Kuhusu suala la Meya
Henry Matata kutoondolewa madarakani RC Ndikilo alisema kuwa hawezi
kulizungumzia suala hilo kw akuheshimu mamlaka ya mahakama na kuwataka chadema
kuvuta subira hadi pale mahakama itakapotoa maamuzi yake.
KAULI YA MBUNGE KIWIA.
Akizungumza katika ofisi
ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Kiwia alisema kuwa waliamua kuitisha maandamano hayo
kutokana na kuelezwa na Waziri Hawa Ghasia kuwa tayari barua hizo zimeishatumwa
mkoani Mwanza.
“Mheshimiwa Mkuu wa mkoa
hawa madiwani waliosimamishw ani wawakilishi wa wananchi,wamekaa nje kwa miezi
saba sasa na uchaguzi wa Meya haukuwa halali ndio maana tuliamua kuitisha
maandamano kwa ajili ya kuhakikisha madiwani hawa wanarejeshwa.
RPC MANGU.
Akizungumza kwa simu juu
ya kutokea kwa vurugu zilizosababisha kupigw akwa mabomu ya machozi,Kamanda wa
polisi mkoa wa Mwanza Ernest Mangu alisema kuwa polisi walifanikiwa kudhibiti
vurugu hizo na hadi sasa hawezi kusema ni wananchi wangapi ambao walikamatwa
kuhusu vurugu hizo.
WANANCHI WAWALAUMU
VIONGOZI NA WANASIASA NA KUWAPONGEZA POLISI.
Baadhi ya wananchi
waliozungumza na Mtanzania juu ya vurugu zilizotokea waliwaonyoshea kidole
wanasiasa pamoja na viongozi wa mkoa wa Mwanza kutokana na kushindwa kusema
ukweli juu ya tukio hilo.
Baadhi walisikika wakisema
kuwa kama barua zipo kweli madiwani hao wanapaswa kupewa na kama azipo basi
walioeneza maneno hayo wachukuliwe hatua kali kutokana na uchochezi.
Wananchi hao pia
walilipongeza jeshi la polisi kutokana na kutumia busara badala ya nguvu
kuhakikisha maandamano hayo yanakuwa ya amani. http://peruzibongo.blogspot.com
Post a Comment