Sheikh Issa Ponda Akiwa mahakamani mkoani Morogoro asubuhi ya leo Sheikh
Ponda Amesomewa Mashtaka Matatu katika Mahakama ya mkoa wa Morogoro
Likiwemo la uchochezi alilolitoa Kwenye Mkutano wa Hadhara Tarehe 10
mwezi huu Ambapo Inadaiwa alisema kwamba
”Ndugu waislamu Msikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za
Misikiti kwani kamati hizo zimeundwa na Bakwata ambao ni vibaraka wa
Serikali ”katika viwanja vya shule ya kiwanja cha ndege Mkoani Morogoro.Baada
ya kusomewa Mashitaka hayo Mahakama imesema Upelelezi Umekamilikaa
Dhamana Imefungwa na Amerudishwa Rumande Mpaka tarehe 28 mwezi huu
ambapo kesi hiyo itaanza kusikilizwa katika Mahakama ya Mkoa wa
Morogoro..Picha Na MATUKIO NA MICHAPO BLOG
Sheikh Issa Ponda Akiondoka mahakamani mara baada ya kusomewa mashtaka matatu na kesi yake imehairishwa Hadi tarehe 28.08.2013
Post a Comment