Mwenyekiti
wa kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Zitto Kabwe (Mb)
akionesha Leseni mpya za Udereva mbele ya wajumbe wa kamati yake wakati
kamati hiyo ilipokutana na Hazina kujadili namna bora ya kukusanya
mapato ya Serikali hususani yale ya makosa ya barabarani kwa kutumia
mfumo wa risiti za ki electroniki kwa kuwa leseni hizo zipo kwenye mfumo
wa kisasa. Kamati hiyo imeileza Hazina jinsi fedha nyingi za makusanyo
mbalimbali zinavyopotea kwa kutumia mfumo wa zamani wa risiti za kawaida
na hata mara nyingine serikali kutofaidika na mapato hayo licha ya
kwekeza zaidi katika mifumo hii.
Mjumbe wa kamati ya Bunge ya PAC Mhe. Gaudensi Kayombo akifafanua jambo mbele ya watendaji wa Hazina wakati wakikao na Kamati hiyo.
Naibu
katibu Mkuu Hazina Bi. Elizabeth Nyambibo akijibu baadhi ya hoja
zilizotolewa na wajumbe wa kamati ya Bunge ya PAC kujadili masalwa
mbalimbali ya utendaji wa wizara hiyo walipokutana na kamati hiyo leo.
Picha na Owen Mwandumbya
Post a Comment