Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA (TMAA) IMETOA WITO KWA UMMA.

 


SONY DSCMkurugenzi Utawala na Fedha Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania(TMAA)Bw,Bruno Mteta(katikati)akiongea na waandishi wa habari leo Ofisini kwake Agosti 23.8.2013 jijini Dar es salaam,kuhusu udhibiti wa utoroshadi na biashara haramu ya madini nchini(kushoto)Afisa Habari(TIMAA)Bw,Yisambi Shiwa(kulia)Mkurugenzi wa Udhamini wa Madini na Huduma za Maabara,Bw Dominic Rwekeza. SONY DSCWaandishi wa habari wakiwa kwenye mkuta wakimsiliza Mkurugenzi Utawala na Fedha Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania(TMAA)Bw,Bruno Mteta,wakati akito tamko kwa Umma kuhusu udhibiti wa utoroshadi na biashara haramu ya madini nchini,ulifanyika leo Ofisini kwake Agosti 23.8.2013 jijini Dar es salaam
PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE DAR ES SALAAM

………………………………………………………………..

Na Philemon Solomon
Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania(TMAA)imetoa wito kwa Umma kujiepusha na shughuli za utoroshaji na biashara ya magendo ya madini kwani hatua kali zitaendelea kuchukuliwa kwa yeyote atakaebainika kukutwa akijishughulisha na utoroshaji wa madini.akiongea na waandishi wa habari leo Ofisini kwake Mkurugenzi Utawala na Fedha Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania(TMAA)Bw,Bruno Mteta.amesema
Moja ya majukumu ya wakala ni kufuatilia na kuzuia utoroshaji magendo ya madini,na ukwepaji wa ulipaji mrabaha kwa kushirikiana na vyombo na mamlaka nyingine husika za serikali”katika kipindi cha kuanzia Septemba 2012 hadi Julai 2013,wakala umeweza kukamata watoroshaji wa madini aina mbalambali katika matukio 23 tofauti ya madini yaliyokamatwa yana thamani ya jumla ya Dola za Marekani 8,231,740,sawa na Shilingi za Kitanzania bilioni 13.17.
watoroshaji hao walikamatwa na wakaguzi wa wakala waliopo katika Madawati ya Ukaguzi wa Madini katika viwanja vya ndege vya Kimataifa vya Dar es salaam,Kilimanjaro na Mwanza.watoroshaji hao walikamatwa na wakaguzi wa Wakala kwa kushirikiana na Taasisi nyingine ambazo ni Mamlaka ya Viwanja vya Ndege(TMAA),Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA),Jeshi la Polisi,Idara ya Uhamiaji na Usalama wa Taifa.watoroshaji hao wengi wao ni raia wa kigeni na wachache ni Watanzania”alisem Mteta
Alitaja matukio ya hivi karibuni,ambapo amesma”Tarehe 20 Agosti,2013,raia mmoja wa kigeni alikamatwa na Mkaguzi wa Wakala kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa na aina mbalimbali ya madini ya vito yenye thamani ya Dola za Marekani 15,826,sawa na Shilingi milioni 25.32.hatua za kisheria zimechukuliwa dhidi yake ikiwa ni pamoja na kuyataifisha madini hayo kuwa mali ya serikali.
Tarehe 20 Agosti,2013,raia mwingine wa kigeni alikamatwa na Wakaguzi wa TMAA kwa kushirikiana na Askali Polisi,Usalama wa Taifa na Ofisi ya Madini kanda ya Mashariki kwenye makazi ya huko Jangwani Beach akiwa na aina mbalimbali ya madini ya vito.Uthaminishaji wa madini hayo unaendelea,japokuwa yanaonekana kuwa na thamani kubwa sana.mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa uchungzi zaidi na hatua za kisheria,vilevile unatoa wito kwa Umma kutoa taarifa kwa wakala pale wanapobaini kuwepo kwa raia wa kigeni au Watanzania wanaojishughulisha  na utoroshaji au biashara haramu ya madini kwa mawasiliano ya haraka,wananchi watumie barua pepe
info@tmaa.go.tz na simu 022-2601819″alisema
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top