Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

BALAA LA ZIARA YA KINANA LILIVYO


 Kinana akishiriki kula chakula cha asili aina ya  mchembe ambacho ni viazi vilivyokaushwa
Nape alkila wali kwa maharage pamoja na wananchi chakula kilichoandaliwa na Balozi kwa ugeni huo
 Wananchi wa Kijiji cha Yoma, Kata ya Somanda wilayani Bariadi, wakishangilia kuonana na Katibu Mkuu wa CCM, Kinana ii asuhishe mgogoro maji ktika kijiji hicho.
Wananchi wakitoa malalamiko yao kwa Kinana na kumuomba auamuru uongozi akiwemo mhandisi wa maji wa wilaya ya Bariadi, kuwapatia haraka maji kutoka kwenye kisima kilichopo katika kijiji hicho.

Kinana akiwasihi wananchi hao kuwa wavumilivu hadi Oktoba muda ambao wameahidiwa na uongozi kuwa wataanza kupata maji.
 Kinana akisaidia kujnga vyoo vya Shule ya Sekondari ya Malambo, Bariadi mjini leo
Mbunge wa Bariadi Magharibi Andrew Chenge akiahidi kujenga moja ya vyumba vya madarasa katika shule ya Malambo
Chenge akielezea katika mkutano wa hadhara ahadi mbalimbali  zilizotekelezwa na yeye pamoja na serikali katika jimbo hili.
Nape akihutubia mkutano wa hadhara mjini Bariadi,mbapo pamoja na mambo mengine aliwashambulia viongozi wa chadema kuhusu kitendo cha kumwandama Balozi wa China nchini, Lu Youqing ambaye amewezesha viwanda kumi vya nguo, mafuta na nyama kujengwa mkoani Shinyanga pamoja na kujenga chuo cha kuboresha zao la pamba. Viwanda hivyo vitakuwa na uwezo wa kuajiri vijana zaidi ya 20,000. 
 Kinana akihutubia wananchini katika mkutano wa hadhara mjini Bariadi, ambapo pamoja na mambo mengine, aliwataka viongozi wanaowatesa waalimu kwa kutowatekelezea maslahi yao, wajuzulu mara moja.
Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria mkutano huo wa hadhara
 Kinana akimkabidhi pikipiki mmoja wa viongozi wa bodaboda zilizotolewa na baadhi ya viongozi wa ccm wialyani humo
Kiongozi wa Bodaboda wilayani Baraiadi, Masumbuko Nchina akiapatiwa na Kinana sh.mil. 1 iliyotolewa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Simiyu, Njalu  Silanga.
Momoja wa wanachama wapya wa CCM, akipatiwa na Kinana  kadi yake ya uanachama katika mkutano huo wa hadhara.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top