Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

maonesho ya Wanasayansi Vijana wa Shule za sekondari Tanzania katika picha


1SAYANSIMwanafunzi Deogratius Daudi wa shule ya Sekondari  Mwembeni kutoka mkoani Mara (kushoto) akimweleza mwamuzi wa maonesho  ya Wanasayansi Vijana wa Tanzania kutoka Kitengo cha Masuala ya Teknolojia  wa ESB International  Edwina O’ Callaghan katika ukumbi wa Diamond Jubilee leo jijini Dar es Salaam. 2 SAYANSIMwanafunzi katika maonesho ya Wanasayansi Vijana wa Tanzania kutoka Kitengo cha Masuala ya Teknolojia  wa ESB International  Edwina O’ Callaghan (kushoto) akisikiliza maelezo juu ya matumizi ya umeme wa mwanga wa jua kwa matumizi ya kupikia kwa kutumia  jiko lililotengenezwa kwa ajili ya kupikia (Oven) kutoka kwa mwanafunzi Deogratius Daudi wa shule ya Sekondari  Mwembeni kutoka mkoani Mara (kulia), katikati ni mwanafunzi Yusuph Tito. 3 SAYANSI 
Mbilimbi ni tunda linalotumika kama chachandu (kiungo cha mboga) kwa ajili ya kuongeza ladha ya chakula, lina uwingi wa asidi (citric acid) ambayo ni muhimu kwa binadam mahususi kwa ajili ya mmeng’enyo wa chakula mwilini. Linatumiwa hasa mikoa ya ukanda wa Pwani ikiwemo Dar es Salaam, Morogoro,Pwani, Lindi na Tanga. Shule ya Sekondari ya Wasichana Kilakala kutoka mkoani Morogoro (imewakilishwa na Irene Maigwa na Betha Shao wote kidato cha sita) kwenye banda lao la maonesho  ya Wanasayansi Vijana wa Tanzania yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee leo jijini Dar es Salaam. 4 SAYANSIMwanafunzi  wa shule ya sekondari ya wasichana Jangwani Liberata Kasekwa (kushoto) akimulezea mwl. Salome Mbago kutoka  shule ya sekondari Morogoro  (katikati) aliyeshikilia chupa nyenye dawa ya kuulia wadudu iliyotengenezwa kwa kutumia limao kwenye maonesho ya Wanasayansi Vijana wa Tanzania yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee leo jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Eleuteri Mangi – MAELEZO)
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top