Mwezeshaji
wa warsha Bw. Mwalimu Wilson-olesira alie simama akizungumza na
washiriki wa warsha ya kujadili mchango wa jamii katika kusaidia watoto
wanaoishi katika mazingira magumu, katika ukumbi wa zamani wa Radio
uliopo Rahaleo Mjini Zanzibar. Warsha hiyo ya siku 1 imeandaliwa na
(ZAPHA +). Afisa
vituo vya kulelea watoto yatima Idara ya Ustawi wa Jamii Zanzibar
Lahdad Haji Chum akichangia katika mjada wa nini tufanye kusaidia watoto
wanaoishi katika mazingira magumu katika warsha ya siku moja
iliyoandaliwa na (ZAPHA +) katika ukumbi wa zamani wa Radio Zanzibar. Maryam
Charles Samwel mmoja ya vijana wanaosaidiwa kimasomo na (ZAPHA +)
akizihamasisha Jumuiya nyengine kusaidia watoto wanaoishi katika
mazingira magumu magumu katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na
(ZAPHA +) katika ukumbi wa zamani wa Radio Zanzibar uliopo Rahaleo Mjini
Unguja. Baadhi
ya washiriki wa warsha ya siku moja iliyo jadili mchango wa jamii
katika kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu, huko katika
ukumbi wa zamani wa Radio Zanzibar uliopo Rahaleo Mjini Unguja.
(Picha na makame Mshenga-Maelezo)
.………..
Maryam Aboud Ali na Riziki Salum Ali
Mkurugenzi
Ofisi wa Elimu Maandalizi Msingi wa Vyuo vya Qur-an Zanzibar amesema
suala la kubuni mbinu shirikishi kwa wadau na wanajamii ndilo ambalo
litasaidia kutoa huduma endelevu kwa watoto wanaoishi katika mazingira
magumu.
Hayo
yalielezwa katika warsha ililoandaliwa na Jumuiya ya watu wanaoishi na
virusi vya ukimwi Zanzibar {ZAPHA PLUS} ililoshirikisha taasisi za
serikali na jumuia za binafsi zinazoshughulikia watoto wanaoishi
katika mazingira magumu iliofanyika katika ukumbi wa zamani wa Redio
Zanzibar.
Aidha
alisema lengo kuu ni kuona changamoto zinazowakabili pamoja na kujua
ni jinsi gani watoto wataweza kusaidiwa na kupatia haki zao za msingi
ikiwemo kivazi, elimu, malaji pamoja na huduma za kiafya.
Kwa
upande wa washiriki katika kongamano hilo walisema kuwa wanahitaji
mashirikiano ya pamoja katika jumuiya mbali mbali’ wanakamati, masheha
wa shehiya na wanajamii kiujumla ili kufikia lengo la kuwakomboa watoto
wanaoishi katika mazing ira magumu. “Watoto wanaoishi katika mazingira magumu tuwakomboe vipi?”walisema washiriki.
Pia
mmoja wa washiriki hao Dadi Ali Chum alifahamisha ipo haja ya kujua
takwimu ya watoto ambao wanaishi katika mazingira magumu ili kuweza
kuzisaidia familia zao.
Jumuia
ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi inahusika na kutetea na kuhimiza
huduma bora za tiba kushiriki katika mapambano dhidi ya ukimwi kutoa
ushauri nasaha na lishe, elimu ya unyanyapaa kwa wanajamii kuhusu
watoto wanaoishi na HIV/AIDS pamoja na kufanyakazi na watoto hao kwa
lengo la kuwapa elimu ya stadi za maisha
Jumuiya
imeweza kuwasaidia watoto 749 wakiwa wanawake 386 nawanaume 360 kwa
Unguja na Pemba katika kuwasaidia na hali ngumu za maisha.
Nae
mratibu wa jumuiya hiyo Mussa Tano Juma alisema kuwa jumuia imeandaa
vipindi mbali mbali kwa jamii ili kufanikisha maendeleo ya watoto hao.
Jumuia
hiyo imeanzishwa mwaka 1994 ikiwa na wanachama 26 ikiwa na klabu moja
ya watoto, na hadi sasa imefanikiwa kuwa na klabu kumi.
Post a Comment