Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) Dr. Mustafa Ali Garu akimpatia
maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hatua
zinazochukuliwa za ujenzi wa tangi la kuhifadhia maji safi liliopo
machui chini ya ufadhili ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB).
Wahandisi
wa Kampuni ya Kimataifa ya ujenzi ya Reli ya Nchini China (CRJ) na wale
wa mamlaka ya Maji Zanzibar wakiwa katika harakati za ujenzi wa Tangi
la kuhifadhia maji liliopo Machui Wilaya ya Magharibi.
Balozi
Seif akipatiwa maelezo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar
(Zawa) Dr. Garu kuhusu hatua za uchimbwaji wa visima vya maji katika
kituo cha Chumbuni unaofadhuiliwa na Serikali ya Ras Al-Khaimah.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akishuhudia upungufu mkubwa wa
maji uliopo katika kianzio cha maji cha chem Chem ya Mwanyanya wakati
alipofanya ziara ya kukagua kuduma hiyo katika maeneo tofauti Unguja.
Moja
ya Baadhi ya mabango yaliyowekwa na Mamlaka ya Maji Zanzibar
kulizunguuka eneo la Chem Chema Mwanyanya kutoa taaluma ya
kutotumiwa kwa ujenzi likionekana kufutwa kabisa na kusababisha uvamizi
wa eneo hilo la hifadhi. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ
**********************************
Wizara
ya Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Zanzibar imeagizwa kuendelea kutoa
Elimu kwa Jamii juu ya umuhimu wa kutunza vianzio vya Maji ili
rasilimali hiyo muhimu itosheleze kuhudumia wananchi wakati wowote bila
ya vikwazo.
Kauli
hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi alipofanya ziara ya kukagua maeneo ya vianzio vya Maji, ujenzi wa
matangi ya kuhifadhia maji pamoja na uchimbwaji wa visima vya
maji Katika maeneo tofauti hapa Unguja.
Balozi
Seif alisema vianzio vingi vya maji hapa nchini hivi sasa vimepunguza
uzalishaji wa huduma ya maji kutokana na maeneo hayo kuvamiwa kiholela
kwa ukataji ovyo wa miti, uharibufi wa mazingira na hata ujenzi wa
nyumba za kudumu usiozingatia taratibu za kisheria.
Alisema
Wizara inayosimamia masuala ya maji ihakikishe elimu inayotoa
inatekelezwa ipasavyo, vyenginevyo hatua za kuchukuliwa dhidi ya wale
wanaokaidi taaluma hiyo ifuatwe kwa vitendo ikiwa ni pamoja na
kuwavunjia majengo yao.
Hata
hivyo Balozi Seif alitanabaisha kwamba wananchi waliopewa eka tatu tatu
hawajakatazwa kuendelea na kilimo katika maeneo hayo muhimu wanafuata
taratibu zilizowekwa hasa katika yale maeneo ya hifadhi ya misitu au
maji.
“
Wizara lazima ichukuwe jitihada za kupambana na hatari hii inayotishia
ustawi wa maisha ya viumbe kwa kutoa lugha ya wazi ya kubomolewa wale
wanaokaidi agizo au maamuru ya Serikali “. Alisisitiza Balozi Seif.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar alifahamisha kwamba Wananchi ni vyema
wakaendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali pamoja na Wizara husika
katika kuona juhudi zinazochukuliwa za kupambana na matatizo ya upungufu
wa huduma za maji nchini linapatiwa ufumbuzi kwa pande zote husika.
Balozi
Seif Ali Iddi aliwapongeza watendaji wa Wizara ya Ardhi, Makazi, Maji,
Nishati na Madini hasa wale wa Mamlaka ya Maji Zanzibar kwa juhudi
wanazozichukuwa za kukabiliana na tatizo la upungufu wa maji ambalo
huleta usumbufu kwa wananchi walio wengi nchini.
Mapema
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar { ZAWA } Dr. Mustafa Ali
Garu alisema mabadiliko ya Tabia Nchi yaliyoikumba Dunia hivi sasa
pamoja na uchafuzi wa mazingira katika baadhi ya vianzio vya maji
yamesababisha kupunguwa kwa kiwango kikubwa cha uzalishaji wa huduma
hiyo hapa Nchini.
Dr.
Garu alimtolea mfano Balozi Seif kile kianzio cha maji cha chem Chem ya
mwanyanya ambacho kilikuwa kikizalisha Lita za Maji Bilioni 3 kwa siku
sawa na asilimia 30% mnamo mwaka 1999 na kushuka hadi lita Bilioni 1.5
kwa siku sawa na asilimia 15% ikiwa upungufu wa nusu ya uzalishaji
uliopo hivi sasa.
Akizungumzia
mradi mkubwa wa maji wa Shilingi Bilioni 67 unaofadhiliwa na Benki ya
Maendeleo ya Afrika { ADB } Mkurugenzi huyo Mkuu wa Mamlaka ya Maji
Zanzibar alimueleza Balozi Seif kwamba mradi huo hivi sasa uko katika
hatua ya miundo mbinu, Taaluma pamoja na upatikanaji wa Vifaa.
Dr.
Garu alisema mradi huo unatarajiwa kukamilika mwezi wa Januari mwaka
2014 kwa hatua za uchimbaji wa visima pamoja na ujenzi wa matangi katika
maeneo mbali mbali Unguja na Pemba.
Alifahamisha
kwamba awamu ya Pili ya mradi huo unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo
ya Afrika { ADB } utahusisha ujenzi wa vyoo katika skuli mbali mbali za
Zanzibar sambamba na uimarishaji wa miundo mbinu ya mitaro ya maji
machafu katika manispaa ya Mji wa Zanzibar.
Kuhusu
mradi wa visima vya maji unaofadhiliwa na Serikali ya Ras Al –Khaimah
Dr. Garu alisema Nchi hiyo imetenga Jumla ya Dola za Kimarekani Milioni
1.5 kugharamia mradi huo utakaosaidia zaidi ya wananchi 200,000 hapa
nchini.
Alieleza
kwamba jumla ya visima 50 vitachimbwa pamoja na ujenzi wa matangi
katika maeneo tofauti ya Zanzibar vikiwemo pia Vijiji vya Kiwengwa,
Kitope pamoja na Kisongoni.
Dr.
Garu aliongeza kuwa katika kukabiliana na tatizo la upungufu wa huduma
za maji safi na salama Mamlaka ya maji Zanzibar kupitia Serikali Kuu
pamoja na washirika wa maendeleo imejipanga kuwa na visima 73 na matangi
ya kuhifadhia maji yapatao 17 unguja na Pemba.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar katika ziara hiyo alipata fursa ya kukagua
na kupata maelezo juu ya visima vinavyotoa huduma vilivyopo Chumbuni
vinavyopeleka maji kituo kikuu cha saateni ambavyo baadhi vimefadhiliwa
na Serikali ya Ras Al – Khaimah.
Pia
aliangalia chem Chem ya maji iliyopo eneo la mwanyanya na kujionea hali
halisi ya upungufu wa uzalishaji wa maji katika kianzio hicho pamoja na
uchafuzi wa mazingira unaolizunguuka eneo hilo la hifadhi ya maji na
kupelekea hata vibango vinavyotoa elimu ya kutotumiwa eneo hilo
vimefutwakwa rangi.
Balozi
Seif akiambatana na Uongozi mzima wa Wizara ya Ardhi, Makazi, Maji,
Nishati na Madini pamoja na Mamlaka ya Maji pia alikagua maendeleo ya
ujenzi wa tangi la kuhifadhia maji litakalokuwa na uwezo wa kuhifadhi
lita milioni 1,500,000 za maji hapo machui chini ya ufadhili wa Benki
ya Maendeleo ya Afrika { ADB }.
Baadaye
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimalizia ziara yake kwa kukagua
harakati za uchimbaji wa visima vya maji safi hapo katika kijiji cha
Tunguu vinavyofadhiliwa na Serikali ya Ras Al – Khaimah.
Post a Comment