Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Mizengo Pinda, akiongea na timu ya Clouds Media Group katika shamba lake
lililopo maeneo ya Zuzu mjini Dodoma. Hiyo ilikuwa ni katika kuonyesha jinsi
gani anavyotumia Fursa ya kujiongezea kipato kwenye kilimo ambapo analima na
kufuga mazao kama vile Zabibu, Migomba, Nyanya, Nyuki, Mbuzi na Kuku wa
kienyeji.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Mizengo Pinda, akiongea na timu ya Clouds Media Group (hawapo pichani) katika
shamba lake lililopo maeneo ya Zuzu mjini Dodoma. Hiyo ilikuwa ni katika
kuonyesha jinsi gani anavyotumia Fursa ya kujiongezea kipato kwenye kilimo
ambapo analima na kufuga mazao kama vile Zabibu, Migomba, Nyanya, Nyuki, Mbuzi
na Kuku wa kienyeji. Pichani kulia ni Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa
Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Mizengo Pinda, akielekeza lilipo shamba la ekari sita la zabibu kwa timu ya
Clouds Media Group lililopo maeneo ya Zuzu mjini Dodoma. Hiyo ilikuwa ni katika
kuonyesha jinsi gani anavyotumia Fursa ya kujiongezea kipato kwenye kilimo
ambapo analima na kufuga mazao kama vile Zabibu, Migomba, Nyanya, Nyuki, Mbuzi
na Kuku wa kienyeji. Zinazoonekana kwa chini pichani ni zabibu zilizovunwa na
kuanikwa juani.
Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Pinda, ambaye mbali na kuwa
na majukumu makubwa ya kitaifa pia mashuhuri sana katika swala la kilimo.
Mheshimiwa Pinda anaonyesha njia na mfano wa kuigwa na vijana kwani ameweza
kuwekeza katika kilimo ambapo ana shamba lenye ekari 50 lililopo mkoani Dodoma
maeneo ya Zuzu.
Timu ya Clouds
Media Group ikiongozwa na mkurugerugenzi wa vipindi na uzalishaji Bw. Ruge
Mutahaba ilipata fursa ya kumtembelea Mhesimiwa Pinda nyumbani kwake mjini
Dodoma siku ya jumamosi majira ya saa mbili asubuhi na baada ya hapo safari
iliyochukua kama dakika 25 hivi kuelekea Zuzu ilianza, wengi hawakuamini kama
shamba kama lile linaweza kuwepo maeneo yale ambapo palionekana ni sehemu yenye
ukame. Shamba la kisasa lenye mazao maarufu kama vile Mizinga ya Nyuki, Zabibu,
Mahindi, Nyanya, Migomba ya kutosha, na mengineyo ikiwemo mbuzi zaidi ya 200 na
kuku wa asili.
Mheshimiwa Pinda
alieleza kwa nia yake ya kujikita kwenye kilimo hasa kwenye ufugaji wa nyuki ni
baada ya kuona kuna ‘FURSA’ nyingi katika ufugaji wa nyuki wa asali, ambapo
asali inauzika sehemu mbalimbali duniani. Mbali na kufuga pia ni mnunuzi mkubwa
wa asali kutoka kwa wakulima wenzake kwani yeye ana kiwanda kidogo cha
kusindika asali “Mimi pia hununua asali kwa wafugaji wenzagu kutoka Manyoni,
Singida na Sikonge kwa sababu nina kiwanda kidogo cha kusindika asali inayoitwa
“Follow the Honey” kutoka Tanzania, ambayo naiuza hapa nchini na nje ya nchi na
inauzika sana”, kazi sio tu kuvaa tai shingoni na kukaa ofisini fursa nyingi
zipo kwenye kilimo”.
“Ukiangalia haina
tofauti na asali nyingine ambazo huwekwa kwenye vidumu vya kawaida, lakini
muonekano wa nje ndio kivutio na kinajenga imani kwa mnunuzi kwamba hii asali
ina kiwango kizuri, huwezi kuuza asali nje ya nchi au kuweka kwenye maduka
makubwa (Supermarket), na hilo tatizo lipo kwenye bidhaa nyingi tu kama vile
mchele, unga wa mahindi, maharage na mengine mengi tu, tumieni FURSA hii ya
kilimo, na sio lazima uingie shambani ulime, mjiunge kikundi mkusanye asali au
mazao kwa wakulima, muweke kwenye mifuko ambayo mtatengeza vizuri ikiwa na jina
la group lenu au jina zuri ambalo limvutia mteja hapo mtauza tu”. Alisema
Mheshimiwa Pinda.
Pinda aliishukuru timu nzima ya Clouds Media Group kwa
kuendesha semina hiyo ya kutoa elimu na kuwahamasisha vijana kujitambua na
kujiinua kiuchumi. Akizungumza na Mheshimiwa Pinda, Ruge Mutahaba alisema “Nia
yetu kwa sasa ni kuwapa vijana elimu kuhusu “FURSA” zilizopo na wazitambue, pia
waweze kuweka akili na mawazo yao sawa kabla ya kuamua, hatua ya pili itafuata
kuwawezesha kupitia mawazo waliyoyapata baada ya hatua ya kwanza” ila kama
ulivyosema mheshimiwa vijana wakiungana na kufanya jambo kwa pamoja wanaweza
kufanikiwa sana, tunakushukuru sana kwa kutualika kwani umetupa moyo kukuona
jinsi unavyoendeleza kilimo kwa vitendo na si nadharia”. Alimaliza Ruge.
Baadhi ya vijana wanaofanya kazi katika shamba hilo
wamemshukuru mheshimiwa Pinda kwa kuwapa ajira na pia wanajifunza mengi kuhusu
kilimo kutoka kwake, Pia kuna vijana 20 wanaoishi jirani na mheshimiwa
wamewasaidiwa kuanza kufuga nyuki, 10 ni wavulana na 10 wasichana kwa sasa
wanaendelea vizuri na ufugaji. Semina hizo ambazo zinaenda sambamba na tamasha
la Serengeti Fiesta zinadhaminiwa na makampuni ya NSSF, Zantel na Maximalipo,
wiki hii itakuwa mkoani Kagera na Shinyanga.
Post a Comment