Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Bodi ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali yazinduliwa rasmi.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akiwasili New Africa Hotel kwa ajili ya uzinduzi wa Bodi ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) leo jijini Dar es Salaam. Kushoto Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel, kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TSN Profesa Moses Warioba.


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel (aliyesimama) akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (aliyekaa kulia), kwenye uzinduzi wa Bodi ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Habari Bw. Assah Mwambene.


Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akihutubia Wajumbe wa Bodi Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) katika hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa New Africa Hotel leo jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali Profesa Moses Warioba akielezea matarajio ya utendaji kazin mara bada ya Bodi hiyo kuzinduliwa rasmi.


Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe na viongozi wengine wa Wizara. Kushoto kutoka kwa Waziri ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel na wa kwanza kushoto ni Kaimu Mhariri Mtendaji wa TSN Bw. Gabriel Nderumaki.
(Picha zote na Benedict Liwenga)
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top