Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

CCM: Msajili wa asasi futa Jukwaa Katiba

Mwanasheria wa CCM, Godwin Kunambi, ameitaka Serikali kufuta usajili wa Jukwaa la Katiba Tanzania kwa sababu linajihusisha na siasa kinyume na sheria.
Alisema Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania, Deus Kibamba, amevunja sheria ya mwaka 2002 kifungu cha 20 kinachokataza asasi za kiraia kijihusisha na siasa.
Kunambi alisema hayo kwenye mkutano wa mkoa wa vyuo vikuu wa CCM na waandishi wa habari.
Alisema mwanzoni mwa wiki hii, Kibamba alionekana akiwa ameshikana mikono na viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani, ikiwa ni ishara ya kuungana kupinga muswada wa sheria ya Katiba usisainiwe na rais.
Alisema wameungana ili kupinga muswada huo usisainiwe na rais na kwamba, Kibamba kwa hilo amekiuka sheria hiyo.
Kunambi alisema alichotakiwa kufanya mwenyekiti huyo ni asasi yake kupinga muswada huo usisainiwe,
bila kuungana na chama chochote. Alishangaa msajili wa asasi za kiraia kutoifuta.

 
MWANANCHI
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top