TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 19. 09. 2013.
WILAYA YA RUNGWE - AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA
KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO
TAREHE 18.09.2013 MAJIRA YA SAA 07:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA KIBISI
BARABARA YA MBEYA/TUKUYU WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. GARI T.470
BMN AKQ AINA YA TOYOTA COASTER LIKIENDESHWA NA DEREVA JAMES S/O
GODFREY, MIAKA 37, MNGONI, MKAZI WA KYELA LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU
NISSA S/O JIMMI, MIAKA 37, KYUSA, MKAZI WA KATUMBA NA KUSABABISHA KIFO
CHAKE PAPO HAPO. CHANZO KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA
HOSPITALI YA MAKANDANA – TUKUYU. DEREVA AMEKAMATWA TARATIBU ZINAFANYWA
ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA
KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA
USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA MBARALI – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
|
MNAMO
TAREHE 18.09.2013 MAJIRA YA SAA 14:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA KUNYWA –
MADIBIRA WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA
WALIMKAMATA JOYCE D/O NYOMI, MIAKA 34, MHEHE, MKULIMA, MKAZI WA KUNYWA –
MADIBIRA NA WENZAKE WANNE [04] WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI
[GONGO] UJAZO WA LITA 10. MBINU NI KUNYWA POMBE HIYO KATIKA KILABU CHA
MTUHUMIWA. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI
ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO]
KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment