Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katikati akiwa
katika picha ya pamoja na Andrew Nyerere Mtoto wa Kwanza wa Baba wa
taifa Mwalimu Julius K. Nyerere wakati alipozuru kaburi la Mwaasisi
huyo wa taifa la Tanzania Mwitongo, Butiama Nyumbani kwa mwalimu Mkoani
Mara jana, Kinana alifanyakazi na Andrew Nyerere
wakati wakilitumikia Jeshi la Ulinzi la wananchi la Tanzania (JWTZ),
Katibu Mkuu huyo jana aliendelea na ziara yake katika wilaya ya Butiama
katika kuimarisha chama na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya
Chama cha Mapinduzi, Kinana ataendelea na ziara yake katika Wilaya ya
Serengeti leo. Kushoto ni Nape Nnayue Katibu wa (NEC) Itikadi Siasa na
Uenezi.PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-BUTIAMA MARA
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiagana na
Andrew Nyerere mara baada ya kuzuru Kaburi la Baba wa Taifa Hayati
Mwalimu Julius K. Nyerere Mwitongo Butiama jana
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa tatu
kutoka kulia akiongozwa na ndgu wa Mwalimu Mzee Jack Nyamwaga wakati
akielekea kuweka shada la maua katika kaburi la Baba wa Taifa Hayati
Mwalimu Julius K. Nyerere jana mjini Butiama, Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya
Butiama Mama Mabula
Katibu
Mkuu wa CChama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katikati
akiweka shada la maua kwenye kaburi la Hayati. Mwalimu Julius K. Nyerere
huku Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi akishuhudia tukio
hilo.
Wana
habari nao wakishiriki kuweka mashada ya maua katika Kaburi la Baba wa
Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere jana kutoka kulia ni Mkurugenzi wa
Mtandao wa Fullshangwe Bw. John Bukuku, Said Mwishehe kutoka Jambo Leo
Oktavian kutoka CCM Gerson Msigwa wa TBC, Ufo Saro wa ITV na Prosper
Dereva wa CCM.
Katibu
Mkuu wa CChama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa pili
kutoka kulia akimsikiliza Balozi Safari wakati alipotembelea Shina
namba 14 Mwitongo Butiama na kuzungumza na wanachama wa shina hilo ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero zao.
Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi akisalimiana na Mzee
Jack Nyamwaga huku katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa pili
kulia akizungumza na mzee Mdogo wa Mwalimu Julius K. Nyerere Daniel
Nyerere mara baada ya kumaliza kikao chake na wanachama katika shina
namba 14 Mwitongo.
Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi CCM kulia akizungumza na
Mh. Nimrod Mkono aka “Mkono kwa Mkono”Mbunge wa Jmbo la Musoma
Vijijini.
Hili
ni Jengo la zahanati ya kata ya Busegwe ambalo ujenzi wake unaendelea
kwa kushirikisha Halmashauri ya wilaya ya Butiama vijijini Mbunge wa
Jimbo la Musoma Vijijini Mh. Nimrod Mkono na nguvu za wananchi.
Katibu
Mkuu wa CChama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki
kupia lipu wakati alipokagua ujenzi wa zahanati ya Busegwe jana kulia ni
Mgendi Sikila mmoja wa mafundi wanaojenga zahanati hiyo.
Katibu Mkuu wa UWT Taifa na Mbunge wa viti maalum kutoka mkoa wa Mara Amina Makilagi akishiriki kubeba udongo, wakati Katibu Mkuu wa CChama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokagua ujenzi wa zahanati hiyo kata ya Busegwe
Katibu Mkuu wa CChama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mganga mkuu wa Wilaya ya Butiama Dk Wilbert Manase wakati alipotembele ujenzi wa zahanati hiyo.
Mbunge
wa Jimbo la Musoma vijijini Mh. Nimrod Mkono akitoa maelezo mbele ya
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akikagua ujenzi wa
zahanati Busegwe
Mbunge
wa Jimbo la Musoma vijijini Mh. Nimrod Mkono akishiriki kucheza ngoma
na moja ya vikundi vilivyokuwa vikitumbuiza katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CChama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimuangalia Katibu Mkuu wa UWT Taifa Bi. Amina Makilagi wakati akishiriki kucheza ngoma.
Mkuu wa Wilaya ya Butiama Mama Mabula akizungumza na wananchi katika kijiji cha Bwai.
Katibu Mkuu wa CChama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
akimshukuru Diwani wa kijiji cha Bwai Jamila Nyamanda kupitia TPP
Maendelea kwa ushirikiano wake katika kutekeleza ilani ya Uchaguzi ya
Chama cha Mapinduzi CCM
Katibu Mkuu wa CChama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
akifurahia jambo wakati alipokuwa akimsikiliza mzee Nyanda Totela
wakati alipokagua Shule ya Msingi ya Bwai Musoma vijijini jana
Shule ya Msingi Bwai inavyoonekana
Nape
Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi CCM kulia akizungumza katika
mkutano wa hadhara uliofanyika jana Kyabakari Butiama jana
Katibu
Mkuu wa CChama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivishwa
mgolole na Katibu wa kabila la Zanaki Mzee Peter Nyamrubwe Nyamrubwe
kama ishara ya kuwa mmoja wa viongozi wa kimila wa kabila la wazanaki,
kulia ni Mh Nimrod Mkono Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini.
Katibu
Mkuu wa CChama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi
baiskeli kwa Gwesani M. Gwesani moja wa makatibu kata waliokabidhiwa
baiskeli hizo kwa ajili ya kuimarisha Chama Wilayani Butiama
Baadhi ya ananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi akiwahutubia wakazi wa mji wa Kyabakari Wilayani Butiama jana
Post a Comment